WANNE MBARONI KWA UUZAJI WA GONGO NA BANGI KATAVI
WATU
wanne mkoani Katavi wamekamatwa kwa makosa tofauti likiwemo la uuzaji wa
Gongo na debe moja la Bangi.
Taarifa
hiyo imetolewa leo na Kamanda wa mkoa wa Katavi Damas Nyanda wakati akizungumza
na Mpanda radio juu ya matukio yaliyotokea mkoani hapa hivi karibuni.
Aidha
Nyanda amewataka wananchi kuacha kujihusisha na biashara haramu kama njia ya
kujipatia kipato badala yake wajishughurishe na biashara halali katika kujipatia
kipato.
Sanjari
na hayo amsisitiza kuwa watuhumiwa wote waliokamatwa watafikishwa kwenye vyombo
vya sheria ili hatua zichukuliwe dhidi yao na iwe fundisho kwa wengine.
Matukio
ya uuzwaji wa madawa ya kulevya na vitu visivyo halali kisheria vimekuwa
vikiuzwa Mkoani Katavi.
Pata habari hii pia kupitia P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments