WAJASILIMALI KATAVI WATAKIWA KUTUMIA ELIMU YA UJASILIMALI WANAYOPATA KUFANYA SHUGHULI ZA MAENDELEO KUJIKWAMUA KIMAISHA
Na.Issack Gerald Bathromeo-Mpanda
WAJASILIAMALI wametakiwa kutumia
elimu ya ujasiliamali wanayopewa katika mafunzo ili kujikwamua kimaisha.
Wajasilimali wanawake baada ya somo la mafunzo ya ujasiliamali(PICH ANA.Issack Gerald) |
Rai hiyo imetolewa na Afisa maendeleo ya jamii wa Halmshauri ya
Manispaa ya Mpanda Bi.Marietha Mlozi kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji Manispaa
ya Mpanda wakati akifungua semina ya
siku tatu ya ujasilimali ambayo inafanyika Mpanda Mjini.
Aidha amewasisitiza kuendelea kuunda
vikundi ili kukidhi vigezo vya kukopesheka katika bajeti ya Halmashauri na
fursa nyingine za mikopo zinapopatikana.
Nao baadhi ya wajasiliali ambao
wameshiriki katika semina hiyo wamesema watatumia elimu ya ujasilimali
wanayopewa ili kufanya shghuli zenye tija.
Semina hiyo ya siku tatu ambayo
imeanza leo inatarajia kumalizika Jumatano ya wiki hii ambapo miongoni mwa
wawezeshaji wa semina hiyo ni Shirika la ANAMED ambao ni muunganiko wa dini
mbalibali hapa nchini.
Hata hivyo changamoto ambayo bado
inawakabili wajasiliamali baada ya mafunzo ni ukosefu wa mitaji,teknolojia ya
kisasa katika ufungashaji wa bidhaa na masoko.
Pata habari hii pia kupitia P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments