HALMSHAURI ZA WILAYA YA MPANDA NA TANGANYIKA ZATAKIWA KUTENGA 5% YA MAPATO KWA AJILI YA WAJASILIMALI VIJANA
Na.Richard Mbeho-Mpanda
HALMASHAURI
ya Wilaya ya Mpanda na Tanganyika zimetakiwa
kutenga asilimia 5 za mapato ya ndani kwa ajili ya kuwasaidia vijana
kuanzisha miradi mbalimbali itakayo wawezesha kujikwamua kiuchumi.
Baadhi ya vijana Wilaya za Tanganyika na Mpanda wakiwa kati mikutano ya hadhara(PICHA NA.Issack Gerald) |
Hayo yamesemwa
na mwenyekiti wabaraza la Umoja wa Vijana wa CCM Bw. Stephano Mwakabafu ambae
pia ni diwani wa kata ya uwanja Ndege katika kikao cha kujadili
changamoto mbalimbali zinazowakbili vijana wa mkoa Katavi.
Aidha Bw. Mwakabafu
amewataka pia vijana hao kuunda vikundi ili kuweza kupatiwa mikopo
itakayowasaidia kuongeza kipato na kuondokana na umaskini.
Kwa upande
wa baadhi ya vijana walioshiriki katika kikao hicho wamesema kuwa viongozi
wamekuwa wakiahidi kuwasaidi fedha lakini hawaoni utekelezaji wake.
Pata habari hii pia kupitia P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments