YALIYOMKUTA ALIYEKAMATWA NA JINO MOJA LA TEMBO MKOANI KATAVI LENYE THAMANI YA SHILINGI MIL.1 HAYA HAPA
MTU
mmoja mkazi wa Mgorokani Matandarani wilaya ya
Mlele mkoni Katavi amefikishwa katika mahakama ya wilaya ya Mpanda kwa makosa mawili tofauti likiwemo la kukutwa
na jino 1 la tembo lenye thamani ya shilingi milioni thelasini.
Akisoma
shtaka hilo mwanasheria wa serikali Bi.Jamira Mzilai mbele ya hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo
Mh.Chigangwa Tengwa amemtaja mshtakiwa kuwa ni Stiven Ndangula (59).
Ameongeza
kuwa mnamo mei 5 mwaka huu katika eneo
la mgorokani wilaya ya mlele mshtakiwa
alikutwa na makosa hayo ambayo ni jino la tembo pamoja na kukutwa na nyara za
serikali bila kibali kutoka kwa mkurugenzi wa wanyamapori.
Hata
hivyo mshtakiwa amekana shtaka hilo na
amerudishwa mahabusu kwa kukosa kukidhi vigezo vya dhamana ambapo mahakama
imeahirisha shtaka hilo hadi
litakapotajwa tena juni 23 mwaka huu kwa ajili ya kusikilizwa.
Vitendo vya watu kukamatwa na nyara
za serikali Mkoani Katavi vimekuwa vikitokea mara kwa mara amabapo hata hivyo
kwa kiasi kikubwa wahusika wamekuwa wakikamatwa.
Mwandishi :Issack
Gerald Bathromeo
Mhariri : Issack
Gerald Bathromeo
Endelea kuhabarika na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments