WATANZANIA WAPYA KATUMBA WATAKIWA KUTOKARIBISHA WAGENI KINYUME CHA SHERIA
WATANZANIA
waliopewa Uraia katika Makazi ya Katumba Halmashauri ya Nsimbo wilayani Mlele,
Mkoani Katavi, wametakiwa kuacha kuwakaribisha watu wanaoingia nchini kinyume
cha sheria.
Rai
hiyo imetolewa na Mkuu wa mkoa wa katavi meja jeneral Mstaafu Raphael Muhuga
wakati akiongea na Watanzania hao wapya Hivi karibuni waishio maeneo ya makazi
ya wakimbizi ya katumba ambapo wametakiwa kuishi kwa Upendo na kuzingatia
Sheria za nchi.
Meja
Mhuga amebainisha kuwa Kumekuwepo na matukio ya Ujambazi hivi karibuni ambapo
mtu mmoja anaedhaniwa kuwa jambazi ameuwawa na wengine wawili kushikiliwa na
jeshi la polisi ambapo mmoja amekimbia na
kutokomea pasipojulikana.
Aidha
mkuu wa mkoa amekemea vitendo vya
watanzania Hao wapya kufanya mazoezi ya kijeshi katika mapori yanayozunguka
makazi hayo kwani kufanya ivyo ni kukiuka taratibu za nchi.
Mwandishi :Issack
Gerald Bathromeo
Mhariri : Issack
Gerald Bathromeo
Endelea kuhabarika na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments