4 HAMAHAKAMANI KWA KUINGIA MGODINI BILA IDHINI YA MMILIKI
WATU wanne wamefkishwa katika mahakama ya mwanzo mjini mpanda
kwa kosa la kuingia mgodini bila idhini ya mmiliki wa mgodi huo.
Akisoma shitaka hilo hakimu mwandamizi wa mahakama hiyo Mh, David Mbembela amewataja
washitakiwa kuwa ni Japhary Mwina [22] Elnest Vitaris[24], Issa Rashidi[ 25]
na Ramadhani Musa[21],wote wakazi wa
Kapanda.
Ameongeza kusema kuwa washitakiwa hao walitenda kosa hilo
February 23 mwaka huu ambapo waliingia katika machimbo ya mgodi wa dhahabu yaliyopo kapanda wilayani mlele na kufanya shughuli zao bila kibali cha
mmliki ambaye ni Shija Sombi .
Kwa upande wao washitakiwa wamekana kutenda kosa hilo na
watuhumiwa wameachiwa kwa dhamana na kesi hiyo imehairishwa hadi hapo itakapo
tajwa tena juni 20 mwaka huu
Mwandishi :Issack
Gerald Bathromeo
Mhariri : Issack
Gerald Bathromeo
Endelea kuhabarika na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments