WITO WA MSTAHIKI MEYA MANISPAA YA MPANDA KWA MADIWANI KUHUSU MADAWATI NA DOMPO LA KUTUPIA TAKA
Mh.Willium Philipo Mbogo amewasisitiza madiwani kusimamia kwa dhati mchakato
wa upatikanaji wa madawati ili ifikapo Mwezi Juni 2016 uwe umeamilika ili kutekeleza agizo la Rais
John Pombe Magufuli kwa wakati mwafaka.
Aidha amemwomba mkurugenzi wa Manispaa
ya Mpanda kusaidia kupatikana dampo kwa ajili ya kutupia taka zinazosombwa
kutoka mjini ili sasa Manispaa iendelee kuwa safi ikiwezekana kuwa Manispaa ya
Kwanza kwa usafi watakapowekwa katika ushindani.
Karibu shule zote Manispaa ya Mpanda
zinadaiwa madawati kati ya madawati 600 hadi 100.
Comments