VIONGOZI SERIKALI ZA VIJIJI NA MITAA MANISPAA YA MPANDA KUANZA KULAMBA POSHO MWAKA WA FEDHA 2016/2017.
Mstahiki
meya Manispaa ya Mpanda,Mh.Willium Philipo Mbogo ameliomba balaza la madiwani
kuidhinisha mpango wa kuwapatia posho wenyeviti wa vijiji na mitaa kuanzia
bajeti ya mwaka wa fedha 2016/2017 unaotarajia kuanza mwezi Julai mwaka huu.
Ombi
hilo amelitoa jana kupitia kikao cha 3 cha balaza la madiwani kilichofanyika
jana Manispaa ya Mpanda.
Mh.Mbogo
amefikia hatua ya kutoa ombi hilo baada ya kujibu swali la mmoja wa wajumbe wa
balaza la madiwani aliyetaka kufahamu ni kwa jinsi au namna gani viongozi wa
serikali za mitaa na vijiji wanafikiria kwa ajili ya posho
Amesema
kuwa haiwezekani wenyeviti wa vijiji na mitaa na viongozi wengine wa serikali
za mitaa waendelee kutopata posho yoyoyte wakati kiongozi wa juu hawezi
kutekeleza na kukamilisha kazi yoyote pasipo huyo kiongozi wa ngazi ya chini
kuhusika asilimia 100.
Ametolea
mfano kwenye kwenye zoezi la usafi,ambapo amesema kuwa mafanikio makubwa
yametokana na jitihada za uzalendo wa viongozi hao.
Kwa
upande wake kaimu mkurugenzi Manispaa ya Mpanda Bw.Lauteri Kanoni amesema kuwa kiasi
cha fedha kitakachopatikana kutokana na uuzwaji wa viwanja zitachangia
kukamilisha asilimia 20 ya mapato ya ndani ya halmashauri ya Manispaa kusaidia
kuwezesha maendeleo ya Serikali za mitaa na vijiji pamoja na viongozi wake kupatiwa posho.
Comments