KILIO CHA WANANCHI WA MTAA WA KAMPUNI KUHUSU SHULE YA MSINGI NSAMBWE CHASIKIKA,WIKI IJAYO KUKABIDHIWA MIL.9 KUKAMILISHA UJENZI WA MADARASA.
Na.Issack Gerald Bathromeo-Katavi
Halmshauri ya Manispaa ya Mpanda
Mkoani Katavi,inatarajia kukabidhi shilingi milioni tisa kwa shule ya Msingi
Nsambwe iliyopo kata ya Misunkumilo kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa madarasa
mawili ya shule hiyo.
Hayo yamebainishwa na Afisa elimu shule
za msingi Bw.Rashid Pilly wakati akijibu swali la Hidary Sumry ambaye ni diwani
wa kata ya makanyagio aliyetaka kufahamu ni lini serikali itakamilisha ujenzi
wa madarasa katika shule hiyo.
Bw.Pilly amezitaja shule za msingi
nyingine zitakazopokea shilingi milioni kumi kila moja wiki ijayo kwa ajili ya
umaliziaji ujenzi wa miundombinu ya madarasa ni pamoja na Mkokwa na Kabwanga.
Manispaa ya Mpanda inatarajia kutoa
kiasi hicho cha pesa kumalizia ujenzi shule ya msingi Nsambwe ikiwa ni
kutekeleza agizo la Mkuu wa Wilaya ya Mpanda alilolitoa hivi karibuni akitaka
Manispaa kutoa pesa kumalizia ujenzi wa madarasa yaliyo usawa wa renta.
Kwa takribani miaka miwili
sasa,wanafunzi wa shule ya msingi Nsambwe wapatao zaidi ya 300 sasa ,wamekuwa
wakisomea chini ya miembe huku wakipata adha ya mvua na jua.
Hata hivyo,suala la ukosefu wa madawati na
vitendea kazi kama vitabu bado ni changamoto ambapo kupitia kikao cha balaza la
madiwani kilichofanyika jana,diwani wa kata hiyo amesema serikali ya kata
inaendelea hushirikiana na wananchi ili kutatu baadhi ya changamoto zilizo
ndani ya uwezo wao.
Comments