WATUMISHI HEWA MPAKA SASA MANISPAA YA MPANDA NI SIFURI PIA KUONGEZA MAGARI MAWILI KWA AJILI YA UZOAJI TAKA
Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda
imesema mpaka sasa haina mtumishi hewa hata mmoja tangu Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Rais Dk.John Pombe Magufuli aziagize Halmshauri zote
nchini kuhakiki watumishi hewa.
Taarifa ya uhakiki wa watumishi hewa imetolewa
leo na Afisa utumishi wa halmashauri hiyo Bw.Rwezaula Justinian wakati akijibu maswali
ya wajumbe wa baraza la madiwani ikiwa ni siku 21 tangu ukomo wa muda wa
uhakiki uliokuwa umetolewa na Rais John Magufuli.
Machi 30 mwaka huu,Mkoa wa Katavi
ulibainika kuwa na watumishi hewa 21 walioisababishia serikali hasara ya shilingi
milioni 20 na laki saba.
Katika
hatua nyingine,wiki ijayo Manispaa ya Mpanda inatarajia kupata gari la pili kwa
ajili ya kuzoa taka huku gari la tatu litakalokuwa likinyonya taka maji likiwa
katika hatua mbalimbali za kupatikana.
Taarifa
ya kupatikana kwa magari hayo imetolewa na Kaimu mkurugenzi Manispaa ya Mpanda
Bw.Lauteri Kanoni.
Aidha
mambo mengine ambayo yamjadiliwa ni pamoja kutafuta ufumbuzi wa migogoro
ya ardhi,uchongaji wa madawati kwa shule
za msingi na sekondari,ujenzi wa vituo vya afya katika maeneo yasiyokuwa na
vituo hivyo,mapambano dhidi ya maambukizi ya virusi vya ukimwi na uwekezaji katika
sekta ya nishati ya umeme na huduma ya maji kwa wananchi ambapo kwa baadhi ya
maeneo ikiwemo kata ya Mpanda Hotel suala la maji limekuwa tatizo ambapo wakazi
wa kata hiyo hawana mabomba wala visima.
Kakao
cha leo ni cha tatu tangu balaza la madiwani Manispaa lianze vikao vyake baada
ya uchaguzi Oktoba 25.
Comments