MKUU WA MKOA KATAVI ATANGAZA KIYAMA KWA MAJAMBAZI
SERIKALI
Mkoani Katavi imesema haitawavumilia watu au mtu atakayehusishwa na Uvunjaji wa
amani ikiwemo kuteka magari Kama ilivyoripotiwa Kutokea hivi karibuni.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa
wa Katavi Meja Jenerali Raphael Muhuga wakati wa Makabidhiano ya nyumba ya
Kituo cha Polisi Kanoge na Nyumba mbili za Askari zenye uwezo wa kukaliwa na
watu wane Zilijengwa kwa Msaada wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kusaidia
wakimbizi UNHCR.
Jenerali Muhuga amesema kuwa kila mtu
anatakiwa kufuata sheria na kanuni za nchi na kuwataka watu kutokujihusisha na
ujambazi na kusisitiza kuwa atakaye kaidi asije akalaumu kwa kile
kitakachompata kutokana na kosa alilolifanya.
Wakati huo huo Mkuu wa Mkoa amewaomba
UNHCR kusaidia vifaa vya kufanyia kazi vikiwemo vyombo vya usafiri ili kufika
kwa urahisi sehemu wanazotakiwa kufika kwa wakati mwafaka.
Kwa Upande wake Mwakilishi wa UNHCR hapa nchini Bi,Chavisa Kapaya Kutoka
Nchini Zambia ameishukuru Tanzania kwa Kuonyesha Ujirani mwema wa Kuwapa
hifadhi wakimbizi Kutoka nchini Burundi Pamoja na Kuwapa Uraia wa Tanzania.
Aidha amewakumbusha raia wapya
kuendelea kutii sheria za nchi ili kuimarisha usalama wan chi.
Kwa upande wa wakazi wa Kanoge yaliyokuwa
Makambi ya wakimbizi Kabla ya kupewa uraia,wameishukuru UNHCR Kutimizi ahadi ya
Ujenzi wa Kituo cha polisi ambacho wamesema Kuwepo kwa kituo hicho itaimarisha
hali ya Usalama katika Makazi yao.
Mwandishi:Meshack Ngumba
Mhariri :Issack Gerald
Comments