MWENYEKITI WA KIJIJI ALIA NA HUJUMA ZA DIWANI,MTENDAJI KUMZUSHIA KUSIMAMISHWA KAZI,YEYE ASEMA AMELETA MABADILIKO MAKUBWA,AJIVUNIA KUTAFUTA ENEO LA UJENZI WA SHULE.
MWENYEKITI wa kijiji cha Muungano
Kata ya Ibindi amekanusha kauli iliyotolewa na Diwani Bw:Jastini Shinje kuwa
amesimamishwa na wananchi kuendelea na wadhifa wake katika kijiji hicho.
Shinje ameviambia vyombo vya habari
kuwa Bw:Makalai Njile ambaye ni mwenyekiti
wa serikali ya kijiji hicho wananchi walimkataa kwenye mkutano wa hadhara kwa
madai ya kuwa chanzo cha mkwamo wa maendeleo.
Hata hivyo Bw Njile amesisitiza kuwa
yeye ni mwenyekiti halali mpaka sasa kwani hajapokea barua yoyote inayotoa
ufafanuzi wa sababu za kumsimamisha na kwamba anacho jua ni uelewano mdogo
uliopo baina yake na diwani huyo.
Mwenyekiti huyo amesema kuwa taarifa
za kupotosha sanjari na hujuma za kutaka kumuundoa katika wadhifa wake
ulitengenezwa na Afisa mtendaji wa kijiji hicho,Bw.Jastini Shinje ambaye ni
diwani wa kata ya Ibindi na wenyeviti wa vitongoji.
Wakati huo huo amesema kwa mwaka
mmoja ambao amekamilisha akiwa madarakani anajivunia kuweka mikakati mingi ya
maenendeleo ikiwemo kutafuta eneo la ujenzi wa shule ya msingi ambayo haikuwepo
tangu uongozi ulipita.
Kwa upande wa baadhi ya wananchi
wamekiri kuwepo kwa migongano ya kiitikadi jambo waliloliita majipu ya mkwamo
wa maendeleo.
Comments