WANNE MBARONI KATAVI KWA KUMILIKI SILAHA SMG,MWENZAO AFA KWA RISASI KATIKA MAJIBIZANO NA POLISI.
Na.Issack Gerald-Katavi
Jeshi la Polisi Mkoani Katavi
linawashikilia watu wanne wakazi wa kata ya Mishamo Wilayani Mpanda
wakituhumiwa kumiliki silaha kinyume na sheria.
Akizungumza na vyombo vya habari Ofisini
kwake,kaimu kamanda wa Polisi Mkoani Katavi SSP Damas Nyanda amesema,watuhumiwa
hao walikamatwa Mnamo Aprili 22 mwaka huu katika kijiji cha cha Bosongola Kata
ya Mishamo wakiwa na silaha aina ya SMG
yenye namba za usajili TX5971-1996 ikiwa
na magazine mbili zenye jumla ya risasi 86 ambapo magazine ya kwanza ilikuwa na
uwezo wa kubeba risasi 31 huku magazine kubwa ikiwa na uwezo wa kubeba risasi 45.
Katika ukamataji huo pia jeshi la
polisi lilifanikiwa kukamata nyama ya kiboko kilo mbili iliyokuwa inapikwa
kwenye sufuria jikoni.
SSP Nyanda amewataja watuhumiwa kuwa
ni James Amos Samandale (28),Amos Maliyatabu Samandale (70),Leoben Kagoma
Karumanzira(25) na Kulwa Joseph Daniel wote wakazi wa Mishamo.
Aidha Kamanda nyanda amesema wakati
msako ukiendelea kufanyika jeshi la polisi walikutana na watuhumiwa watatu
wakiwemo Harumkiza (28),Kulwa Joseph Daniel na mwenzao ambaye bado anatafutwa
ambapo watuhumiwa hao walikataa amri ya askari iliwataka kusimama na badala
yake kukazuka majibizano baina ya askari polisi na watuhumiwa hao na hatimaye Harumkiza
Joshua akapigwa risasi na kufa papo hapo.
Mwili wa marehemu uliokuwa umelazwa
katika hospitali ya Wilaya ya Mpanda ulikabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya
taratibu za mazishi baada ya uchunguzi kufanyika.
Watuhumiwa wanatarajiwa kufikishwa mahakamani
mara baada ya upelelezi kukamilika
Halikadhalika katika majibizano hayo
ya risasi,pikipiki moja yenye namba za usajili T241CKZ SANLG pamoj na kitambulisho
cha kupigia kura vilivyobainika kuwa mali ya mtuhumiwa aliyetoroka vilikamatwa.
Hata hivyo Kamanda amewaonya wananchi
wanaomiliki silaha kinyume na sheria ambapo pia ametoa wito kwa wananchi
kuendelea kutoa taarifa za uharifu ili udhibitiwe kabla ya kusababisha madhara
kwa jamii.
Comments