ZIMAMOTO NA UOKOAJI KATAVI WAELEZA MIKAKATI KUPAMBANA NA MAJANGA YA MOTO
Na.Issack Gerald-Katavi
JESHI la zimamoto Mkoa wa Katavi
limedhamilia kuendelea kutoa elimu kwa jamii kuhusiana na kujiahadhari na
majanga ya moto.
Hayo yamebainishwa na Mkaguzi
msaidizi wa zimamoto mkoa wa Katavi Bw.Edward Kakwale wakati mikakati ya jeshi
hilo katika kupambana na majanga ya moto Mkoani Katavi.
Kakwale amezitaja baadhi ya
changamoto zinazokwamisha ufanisi wa jeshi hilo kuwa ni elimu ndogo kwa jamii
kuhusu namna ya kuzima moto, pamoja na miundo mbinu mibovu ya bara bara hali
inayo pelekea kutofika mapema eneo la tukio.
Aidha ametoa wito kwa taasisi za
kiserikali na zisizokuwa za serikali, pamoja na migodi kuchukua taahadhari kujikinga
na madhara ya moto.
Jeshi la zimamoto lilianzishwa rasimi
2007 ambapo liliingizwa moja kwa moja katika wizara ya mambo ya ndani na
kurithi kazi za Kikosi cha zimamoto kilichokuwa chini ya halmashauri za miji.
Mapema mwezi Aprili,jeshi la polisi
Mkoani Katavi lililaumiwa kwa kuchelewa kutoa huduma ya kuzima moto wakati bweni
la wavulana la shule ya Sekondari Sanny lilipokuwa likiungua ambapo moja ya
changamoto waliyoibainisha ni kutokuwa na maji ya kutosha yaliyosababishwa na
uhaba wa magari na maji kuwa umbali mrefu kutoka tukio la moto.
Comments