WAFANYABIASHARA WAIOMBA SERIKALI KUPANGA KODI NA FAINI INAYOENDANA NA BIASHARA ZAO
Wafanyabiasha wa mazao
ya chakula Mkoani Katavi wameiomba
serikali kupanga kodi na faini kulingana na biashara zao.
Wakizungumza na mpanda
radio wamesema wamekuwa wakilipa fedha
nyingi mamlaka ya mapato Tanzania TRA na
kupelekea kukosa faida .
Wameongeza kuwa
kufuatia ukusanyaji huo imewaasili hasa
kwa kulipa kodi hiyo na hatimae
kucheleweshwa kufunguliwa biashara zao
kwa wakati husika.
Kwa upande wake meneja
wa mamlaka ya mapato Tanzania mkoa wa
TRA Bw.Maiko Temu amesema mwisho wa kulipa kodi ilikuwa ni mwezi February 30
mwaka huu lakini baadhi ya wafanyabiasha
hawakuweza kulipa.
Ametoa wito kwa
wafanyabiasha wote wa mkoa wa Katavi kulipa kodi hiyo kwa wakati.
Comments