WAFANYABIASHARA MPANDA WAPEWA SIKU 21 KUHAMA MAENEO YASIYO RASMI KIBIASHARA
MKUU wa wilaya ya Mpanda Mh Paza Mwalima ametoa siku 21 kwa
wafanyabishara wote wanaofanya shughuli za kiabiashara katika maeneo yasiyo
rasimi kuondoka malamoja.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa wilaya Afisa tarafa wa kata
ya Kashaulili wakati wa ufumbuzi wa mgogoro wa wafanya biashara waliopo eneo la
Nsemulwa katika kata ya Uwaja wa Ndege amesema nilazima wafanya biashara
wafuate taratibu zote za uaanzishaji wa masoko.
Kwa upande wao wafanyabiashara wamedai kusikitishwa na
maamuzi hayo kwani muda uliotolewa ni mfupi nab ado hakuna tamko rasimi kuhusu
wapi wanapaswa kuhamia.
Ni wiki ya pili tangu wafanya biashara wadogo wadogo
waandamane mpaka ofisi za mkuu wa wilaya kwa madai ya kuwepo kwa ubabaishaji
katika zoezi la kuwaondoa wafanya biashara wote walio katika eneo lisilo lasimi
maalufu kama kwa mkumbo.
Comments