MATUKIO MAKUU 11 YA WIKI YALIYOTOKEA NDANI NA NJE YA KATAVI APRILI 4-9,2016
MPANDA-APRILI 04
WAZIRI
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amemuagiza katibu tawala wa
mkoa wa Katavi Bw Paul Chagonja
kufuta uongozi wa mpira wa miguu KAREFA na kusimamia zoezi la uchaguzi wa
viongozi wapya baada ya kufuta uliokuwepo.
Aidha
ameahidi ukarabati wa uwanja wa mpira wa miguu utakao endana na hadhi ya mkoa.
Waziri
Nauye mara baada ya kuwasili jana Mkoani Katavi akitokea Mkoani
Rukwa,amezungumza na wadau mbalimbali wa habari utamaduni sanaa na michezo
ikiwemo viongozi wa serikali ya mkoa wa Katavi katika ukumbi wa idara ya maji
mjini mpanda.
Amesema
lengo la ziara yake katika mikoa mbalimbali ikiwemo mkoani ni kutaka kuishusha
wizara yake mikoani ili kutekeleza majukumu ya wizara hiyo kiurahisi.
Kiongozi huyo kwa
mara ya kwanza tangu ateuliwe kushika wadhifa huo amewasili mjini mpanda majira
ya saa 9 mchana akitokea mkoani Rukwa.
Katika hatua
nyinginea alisema kuwa ameamua wizara yake kuipeleka mikoani hususani mikoa ya
pembezoni mwa nchi ili kushughulikia matatizo yaliyo chini ya Wizara yake.
Waziri
Nape Aprili 6 aliondoka mkoani Katavi kuelekea mkoani Kigoma na hatimaye mkoani
Kagera katika ratiba yake ya kufanya ziara katika mikoa ya pembezoni mwa nchi.
AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUTISHIA KUUA
NA KUSUDIA KUMZIKA ATAKAYE MUUA PORINI MAHALI KUSIKOJULIKANA.
MTU mmoja mkazi wa kashaulili manispaa ya Mpanda
amefikishwa mahakama ya mwanzo mjini Mpanda kwa kosa la kutishia kuuwa kwa
maneno.
Akisikiliza kesi hiyo hakimu mkazi Bw Syliverster Felix Makombe amemtaja mshtakiwa
huyo kuwa ni Bi Sesilia Itoela (26) ambaye
alitenda kosa hilo machi 15 mwaka huu.
Hakimu Makombe amesema mstakiwa alimtishia Bi
Godiliva Ngomalala kuwa atampiga hadi
kumuua na kumzika polini kusiko jilikana.
Hata hivyo mahakama imeahilisha kesi hiyo hadi
itakapo sikilizwa tena april 19 mwaka huu.
WAKAZI KIJIJI CHA KASEGANYAMA MPANDA WAIOMBA SERIKALI KUTATUA MGOGORO
WA ARDHI DHIDI YAO.
WANANCHI
waishio kijiji cha kaseganyama kata ya
kasekese wilaya ya Mpanda wameiomba serikali kutatua mgogoro wa
ardhi unaowakabili katika eneo hilo.
Wakizungumza
na mpanda radio kwa nyakati tofauti wananchi hao wamesema kuwa ni mda mrefu
tangia serikali itoe agizo la kuwataka waondoke tangu mwezi disemba mwaka jana
bila kuonyeshwa maeneo mbadala.
Kwa
upande wake mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho Bw.Kassimu Legi amesema wako
tayari kuhama endapo watapatiwa udhibitisho wa kijiji hicho kuwa kipo au laa.
Hata
hivyo mkuu wa wilaya Mh.Pazza Mwamlima amesema anafahamu suala hilo nakuwa
serikali imepanga ziara ya kwenda kuzungumza na wananchi hao ikiwa ni pamoja na
kuwaelekeza mipaka halisi ya kijiji hicho.
KUTOKAMILIKA
UJENZI WA SHULE YA MSINGI NSAMBWE WILAYANI MPANDA WANANCHI WAIANGUKIA SERIKALI.
MPANDA-April 4
BAADHI ya wakazi
wa mtaa wa kampuni manispaa ya mpanda wameiomba serikali kumalizia ujenzi wa
shule ya msingi Nsambwe.
Wakizungumza na
Mpanda radio kwa nyakati tofauti wakazi
wameelezea kusikitishwa kwao na kutokamilika kwa ujenzi huo kama ilivyo
ahidiwa na serikali kuwa ujenzi huo ungekamilika mwezi march mwaka huu.
Kwa upande wa
mwalimu mkuu wa shule hiyo Cassian Challe,amesema shule hiyo kwa sasa ina jumla
ya wanafunzi zaidi ya miambili wanaosomea katika mahema na kukalia matofali.
Mwaka mmoja
umeisha toka manispaa ya mji wa mpanda ikili kuwepo kwa mkondo huo na kuahidi
kulifanyia kazi suala hilo.
Posted By:Issack Gerald | At:Thursday, April
07, 2016
Na.Issack
Gerald-Katavi
KIKOSI
cha usalama barabani Mkoani katavi
kimesema kimefanikiwa kupunguza ajali za
barabani kwa kutumia kifaa maalum cha kupima mwendo kasi.
Kauli
hiyo imetolewa na mkuu wa usalama barabani Mkoani Katavi Bw John Mfinanga wakati akitoa takwimu za ajali
barabarani kuanzia mwezi January
hadi April mwaka 2016.
Hata
hivyo amesema kuwa kifaa hicho
kina uwezo wa kupima madereva
ambao wamelewa wakati wakiwa barabarani.
Aidha
kikosi hicho kimekuwa kinatoa elimu na kuwashauri watu wanaotumia kilevi kuacha kabisa wanapokuwa wanaendesha vyombo
vya moto.
Pia
ametoa wito kwa jamii kutoa taarifa kwa jeshi la polisi pindi wanapoona dereva
anaendesha kwa mwendo kasi au akiwa na dalili za kutumia kilevi ili kulinda
usalama wa abiria.
Amesema
kuwa katika kipindi hicho cha miezi mitatu ni ajali nne ambazo zimetokea
zikihusisha pikipiki huku katika kipindi kilichopita ajali zilikuwa zaidi ya
hapo.
Aprili 07,2016
MKUU
wa mkoa Meja Jeneral Raphael Muhuga amefanya ziara ya kuitembelea hospitali ya
wilaya ya Mpanda kwa lengo la kutazama changamoto zinazoikabili hospitali hiyo.
Akizungumza
jana na wahudumu katika hospitali hiyo mkuu huyo wa mkoa amesema,moja ya
changamoto alizozibaini ni uhaba wa dawa, Madaktari,wauguzi,uchakavu wa
majengo.
Jeneral
Muhuga amesema serikali imetenga kiasi
cha shilingi BIL.2 kwa ajili ya ujenzi wa hospital ya mkoa ili kuepusha
msongamano unaoweza kujitokeza ikiwa ni pamoja na kuondoa tatizo la wagonjwa
wawili kulala kitanda kimoja.
Aidha
ametoa rai kwa wananchi wanaojichukulia sheria mkononi kwa kuwapiga madaktali wanaotoa huduma kuacha mara moja
kwani kwa kufanya hivyo ni kuvunja sheria ya nchi.
Wakati
huo huo Mkuu wa Mkoa ametembelea chuo cha afya ambacho kina lengo la kutoa mafunzo kwa wanganga
wasaidizi ili kutatua tatizo la upungufu wa wanganga.
Naye
Mhandisi anayejenga chuo hicho amemhakikishia Mkuu wa mkoa kumaliza ujenzi huo
ifikapo mwezi juni mwaka huu.
Kwa
upande wake kaimu mganga mkuu wa hospitali ya wilaya Bw.Benard Kamande amesema
Hospitali hiyo inakabiliwa na ufinyu wa bajeti kuhudumia mkoa mzima wa
Katavi,ubovu wa magari ya kubeba wagonjwai pamoja na upungufu wa wahudumu 157.
AHUKUMIWA JERA MIAKA 4 AU KUTOA FAINI YA MILIONI MOJA NA LAKI MBILI KWA TUHUMA ZA KUKAMATWA NA KICHWA NA NYOKA AINA YA KOBLA NA PEMBE YA INSHA,YUPO PIA ALIYEFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUTISHIA KUUWA
MPANDA-Aprili
08
MAHAKAMA
ya wilaya ya Mpanda mkoani Katavi imemuhukumu mtu mmoja kwenda jera miaka minne
au kulipa faini ya shilingi milioni moja na laki mbili.
Hakimu
mkazi wa mahakama hiyo Bw Chiganga Tengwa amemtaja mtuhumiwa kuwa ni Bw Joseph Mwananoni (70) ambaye
alikamatwa na kichwa cha kobla pamoja na pembe ya insha vyenye thamani ya
shilingi milioni moja.
Tengwa
amesema mshtakiwa alikamatwa
na askari wa jeshi la polisi
katika kituo cha basi akijiaanda kusafirisha nyara hizo.
Kufuatia
hukumu hiyo mahakama imetoa onyo kali na
fundisho kwa jamii kuacha kujihusisha na vitendo vya ujangiri.
Richa
ya juhudi zinazo fanywa na askari wa wanyama poli kwakushirikiana na jeshi la
polisi bado vitendo vya uwindaji halamu na ujangiri vinaendelea.
Wakati
huo huo watu wawili wamefikishwa katika mahakama ya wilaya ya Mpanda kwa
kutuhumiwa na wizi wa katoni za soda zenye zaidi ya thamani ya shilingi milioni
kumi na moja mali ya Sadamu Ally.
Akisikiliza
kesi hiyo hakimu mkazi Bw chiganga tengwa amewataja washtakiwa kuwa ni
Ramadhani Juma na Abubaida wakazi wa
manispaa ya Mpanda.
Tengwa
amesema mnamo tarehe 13 mwezi wa 12
mwaka jana washtakiwa walikutwa na hasara hiyo na miliki wao ndipo alipo
wachukulia hatua.
Ikiendelea
kusikiliza ushahidi kutoka upande wa mlalamikaji mahakama imeahilisha shtaka
hilo hadi litakapo tajwa tena Aprili 18 mwaka huu.
SERIKALI
YAZINDUA UJENZI WA BARABARA KUTOKA MPANDA KUELEKEA TABORA KWA KIWANGO CHA LAMI
KILOMITA 342.9,PIA UJENZI WA BARABARA KUTOKA MBINGA HADI MBAMBA BAY MKOANI
RUVUMA NAYO WAZINDULIWA.
KATAVI-Aprili
08
SERIKALI
imezindua rasmi ujenzi wa barabara ya Mpanda-Tabora yenye urefu wa kilomita 342.9
kwa kiwango cha rami ikiwa ni utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa
barabara kutoka Mpanda mkoani KATAVI hadi Pangale Tabora.
Uzinduzi
huo umetekelezwa na mkuu wa mkoa wa Katavi Meja General mstaafu Raphael Muhuga,kwa
niaba ya Waziri wa Ujenzi,uchukuzi na mawasiliano Mheshimiwa Profesa Makame
Mbarawa katika halfa iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo mkuu wa mkoa
wa Tabora Mh. Aggrey Mwanri
Mh.
Muhuga amesema Barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 342.9 itauganisha kanda 3
za nyanda za juu kusini,kanda ya ziwa na
ukanda wa mashariki.
Wakati
huo huo Mkuu wa Mkoa Muhuga ametoa wito kwa viongozi mbalimbali ili kufanikisha
utekelezaji wa ujenzi wa barabara hiyo ikiwemo kuzingatia ulipaji fidia kwa
wakazi watakaopitiwa na mradi huo katika maeneo yao.
Mwakilishi
wa benki ya maendeleo ya Afrika Bi.Helene Minja amesema kuwa kiasi cha zaidi ya
trilioni 2 kimetengwa kutumika katika ujenzi wa barabara hiyo ambayo ni njia
muhumu ya maisha ya watu wa Katavi.
Kwa
upande wake Mhandisi toka TANROADS aliyekuwa mwenyekiti wa uzinduzi huo, Bw.
Patrick Mfugale amesema kujengwa kwa barabara hizo kutaongeza kasi ya
maendeleo.
Bw.Mfugale
ametaja baadhi ya changamoto ambazo zimekuwa zikijitokeza katika barabara ya
Mpanda kuelekea Tabora ni pamoja na Wizi.
Mbali
na uzinduzi wa ujenzi wa barabara kutoka Mpanda hadi Tabora,uzinduzi huu pia
umekwenda sambamba na uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya kutoka Mbinga hadi
Mbamba Bay yenye kilomita zaidi ya 60.
Ufunguzi
huo umehudhuliwa na viongozi Mbalimbali wakiwemo Mkuu wa Mkoa wa Tabora
Mh.Agrey Mwanri,Waheshimiwa wabunge,wenyeviti wa Halmshauri zilizopo Mkoani
Katavi,Mkuu wa Wilaya ya Sikonge na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma.
Aprili
2,2016,Waziri wa ujenzi,uchukuzi na mawasiliano Profesa Makame Mbarawa alifanya
ziara ya kuangalia changamoto za miundombinu ya barabara mkoani Katavi ikiwa ni
pamoja na kutembelea daraja la mto Koga
Ujenzi
wa baraba hizi ni moja ya utekelezaji wa ahadi ya Rais wa Tanzania Rais John
Pombe Magufuli ambayo aliitoa wakati wa Kampeni za uchaguzi mwaka 2015 ambapo
pia mapema mwezi Februari mwaka 2015 wakati akiwa waziri wa ujenzi wa
miundombinu alikuwa ameahidi ujenzi wa barabara hiyo ikiwa ni pamoja na reli
kutoka Mpanda kuelekea Karema.
Mkoa
wa Katavi ni miongoni mwa mikoa michache nchini, ambayo hadi sasa
haijaunganishwa na mikoa mingine kwa barabara za lami tangu mwaka 1961
Tanganyika ilipopata Uhuru.
NJE YA KATAVI
Aprili
08,MKUU wa Mkoa wa Rukwa, Zelothe Steven amemwagiza Kamanda wa Polisi mkoa huo,
Jacob Mwaruanda kuwasaka na kuwakamata watumishi hewa 18 waliobainika katika
uhakiki uliofanyika katika halmashauri zote mkoani humo hivi karibuni.
Pia
ameagiza fedha hizo zilizolipwa kwa watumishi hao hewa na kuiingizia hasara
kubwa Serikali zirudishwe mara moja.
Akifafanua
alisema katika uhakiki huo, watumishi hewa tisa walibainika katika wilaya ya
Nkasi, wanane katika Manispaa ya Sumbawanga na mmoja wilaya ya Sumbawanga
wakati Kalambo ikiwa haina mtumishi hewa.
Uhakiki
huo unatokana na maagizo aliyotoa Rais John Magufuli baada ya kuwaapisha wakuu
wa mikoa aliowateua, aliwaambia wakafanye kazi ya kutatua kero za wananchi na
sio kwenda kufanya siasa.
Pia
Rais Magufuli aliwapa wakurugenzi wa halmashauri siku 15 wawatoe katika orodha
ya malipo ya mshahara wafanyakazi hewa wote katika halmashauri zote nchini.
Zelothe
alitoa agizo hilo jana katika kikao maalumu cha kufahamiana kilichojumuisha
wazee , viongozi wa dini , watendaji wa umma na wajumbe wa kamati ya ulinzi na
usalama ya mkoa huo kilichofanyika mjini hapa. Akisisitiza kuwa hajaridhishwa
na uhakiki huo, hivyo akaagiza halmashuri zote kurudia upya uhakiki wa
watumishi.
Aliongeza
kuwa aliporudi mkoani humo na kuripoti kazini katika siku yake ya kwanza
ofisini alikabidhiwa kitabu chenye orodha ya watumishi wa umma wa halmashauri
zote akielezwa kuwa hakuna mtumishi hewa katika mkoa wa Rukwa.
RAIS MAGUFULI ATEUA MKUU WA WILAYA HAI
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Bw.
Gelasius Gaspar Byakanwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Mkoani Kilimanjaro.
Taarifa
iliyotolewa leo Ikulu Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John
Kijazi, imeeleza kuwa uteuzi huo umeanzia tarehe 08 April, 2016.
Bw.
Byakanwa anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Antony Mtaka aliyeteuliwa kuwa
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu.
Kabla
ya Uteuzi huo, Bw. Byakanwa alikuwa Katibu wa Rais Msaidizi Mwandamizi.
Uteuzi
huo ameufanya ikiwa ni siku moja baada ya kurejea kutoka nchini Rwanda
alikokuwa akifanya ziara ya siku mbili.
Asante kwa kuchagua P5 TANZANIA MEDIA
Comments