ZIARA ZA WABUNGE WA KATAVI ZASHIKA KASI KATAVI,MBUNGE VITI MAALUMU ACHANGIA SOLA KITUO CHA AFYA MPANDA
Na.Issack Gerald-Mpanda
Kituo
cha afya cha Mwangaza kinachomilikwa na manispaa ya Mpanda mkoa wa katavi
kimekuwa na changamoto mbalimbali ikiwemo
kukosekana kwa vitendea kazi na kupelekea wagonjwa kukosa humuma iliyo bora.
Hayo
yamebainishwa na wajumbe wakamati ya bodi ya manispaa pamoja na wananchi
waliohudhuria katika ziara ya mbunge wa viti maalumu kupitia CHADEMA Bi.Roda
Kunchela katika ziara aliyoifanya kituoni hapo.
Wamesema
kuwa wanahitaji umeme wa ziada ili kuondoa changamoto ya kukosekana kwa umeme unapokuwa umekatika.
Akijibu
na kutolea ufafanuzi changamoto hizo Mh.Kunchela
amesema amesikitishwa na swala hilo ambapo alijitolea amekabidhi Sola kwa ajili
ya kutatua changamoto hiyo.
Aidha
amewaahidi kutatua changamoto ambazo zinahitaji utatuzi wa haraka na kuwataka wafanyakazi kufanya kazi kwa wito
ili kuhudumia jamii inayo wazunguka.
Kwa
sasa wabunge wote wa Mkoa wa Katavi wanaendelea na ziara katika maeneo
mbalimbali kusikiliza kero za wananchi.
Comments