UJUMBE WA VIONGOZI WA KITAIFA MRADI WA ELIMU JUMUISHI WAWASILI KATAVI KWA ZIARA,WAZUNGUMZA NA KAMATI YA KULEA BALAZA LA WATOTO CHANGAMOTO ZAIBULIWA
NA.Issack Gerald-Mpanda Katavi
Kamati ya kulea balaza la watoto
wanaoishi katika mazingira magumu yenye mradi ujulikano kama mradi wa elimu
Jumuishi Wilayani Mpanda Mkoani Katavi,wamekutana leo na kujadili masuala
mbalimbali ikiwemo namna ya kuwasaidia watoto wenye mahitaji maalumu.
Kwa mjibu wa Mkurugenzi wa Shirika la
IAS Tanzania Bi.Elizabert Mavoa ambaye ametembelea kamati hiyo,amesema lengo la
ziara ni kupata taarifa mbalimbali ili kufahamu changamoto zinazowakabili
watoto wenye mahitaji maalumu katika mikoa ya Rukwa na Katavi.
Kwa upande wake Mratibu wa mradi wa
elimu Jumuishi Tanzania Bi.Irene Shayo
ameiasa kamati kushirikisha jamii na serikali kutatua changamoto za watoto
wenye ulemavu.
Naye mratibu wa mradi wa elimu
jumuishi katika mikoa ya Rukwa na Katavi Bw. Joseph Ndomba amesema kuwa katika
Mkoa wa Rukwa na Katavi tangu kuanzishwa kwa mradi katika mikoa hii mwaka 2012,kuna
mafanikio makubwa ikiwemo idadai ya wanafunzi wenye ulemavu kuongezeka shuleni
ili kupata elimu kama watoto wengine
wasio walemavu.
Wakati huo huo,katika kuhakikisha
kuwa wanatatu changamoto ya vitendea kazi,mradi wa elimu jumuishi umepatiwa
zana mbalimbali ikiwemo gari na vifaa vingine ambapo mradi huu hufanya kazi
katika Wilaya za Mpanda,Nkasi na Sumbawanga.
Mradi wa elimu Jumuishi wa awamu ya
pili ulianza mwaka 2015 mbapo kila mradi hudumu kwa kipindi cha miaka 3 kabla
ya kusaini mkataba wa mradi mwingine.
Mpaka sasa tangu mwaka 2012,mikoa
pekee ya Katavi na Rukwa ndiyo mikoa iliyopewa kipaumbele kwa mradi wa elimu
jumuishi.
Mwaka jana 2015,jumla ya wtoto 62
wenye mahitaji maalumu Wilayani Mpanda waliokuwa hawapewi kipaumbele,
waliibuliwa na kupelekwa shuleni kusoma.
Kamati ya balaza la mradi wa elimu
jumuishi Wilayani Mpanda,inafanya kazi chini ya ufadhili wa mashirika matatu
yaliyoungana na kuunda umoja wao unaojulikana kama IFI.
Mashirika
haya ni International Aids
Services(IAS),Free Pentekoste Church Of Tanzania(FPCT) na International Center
Of Disabilities
Comments