WIKI YA MAJI KATAVI,WANANCHI WATAKA MAADHIMISHO YATUMIKE KUWALETEA MAJI SAFI NA SALAMA.
Na.Issack Gerald-Katavi
BAADHI
ya Wakazi wa Manispaa ya Mpanda wameiomba Serikali kutatua changamoto ya maji
inayowakabili katika maeneo yao.
Wakizungumza
juu ya Wiki ya maji wakazi hao wamesema, wanakabiliwa na changamoto ya uhaba wa maji safi na salama.
Kwa
upande wake Mhandisi wa Maji Mkoani Katavi Geraldine Mwamasangula amekiri
kuwepo uhaba huo, na kufafanua kuwa
Serikali imejipanga kutatua
changamoto hiyo.
Amesema
serikali iko mbioni kukamilisha ujenzi wa Mantaki 2 ya maji ya Ikolongo yenye ujazo wa lita million moja
kwa kila tanki yatakayosaidia kutatua changamoto hiyo
Aidha
Mhandisi Mwamasangula amewataka wananchi kuzingatia utunzaji wa vyanzo vya
maji, na kutumia maji kwa uhangalifu.
Mwezi
uliopita,Mkurugenzi wa idara ya maji Mkoani Katavi Injinia Zacharia
Nyanda,alikuwa amesema kuwa kuanzia mwezi machi mwaka huu,zoezi la utandazaji
wa mabomba mapya utaanza ambapo kwa mjibu wa Injini huyo wa maji Mkoani Katavi
mradi huo haujaanza kutokana na uhaba wa pesa.
Wiki
ya maji katika mkoa wa Katavi ilizinduliwa machi 16 ambapo maadhimisho haya
Kitaifa huadhimishwa kila mwaka ifikapo
Machi 16 na kilele chacke machi 22 .
Comments