DIWANI AWAMWAGIA SIFA WANANCHI WAKE USHIRIKI WA SHGHULI ZA MAENDELEO.
Na.Alinanuswe Edward
WAKAZI
wakata ya makanyagio manispaa ya Mpanda wameonyesha mwamko wa ushiriki katika
shughuri za maendeleo kupitia utekelezaji wa mpango wa elimu bure.
Hayo
yamesemwa leo na Diwani wa kata hiyo Mh.Haidary Sumry alipokuwa akizungmzia kuhusu
utekelezaji wa sera ya elimu bure.
Katika
hatua nyingine Diwani huyo,amezitaja baadhi ya changamoto zinazoikabili shule
ya msingi Katavi kuwa ni uhaba wa madawati pamoja na vyumba vya madarasa ambapo
amewaomba wadau na wananchi kwa ujumla kuguswa
na jambo hilo.
Tangu
serikali ya awamu ya tano kutangaza elimu bure kumekuwa na changamoto nyingi
zinazotokana na ongezeko la idadi ya wanafunzi.
Katika
Manispaa ya Mpanda kumekuwa na ongezeko kubwa la wanafunzi walioandikishwa
kuanza darasa la kwanza ambapo mfano wa shule moja yenye wanafunzi wengi katika
Manispaa yam panda ni Shule ya Msingi Nsemulwa yenye wanafunzi zaidi ya 2000
huku darasa la kwanza na chekechea pekee wakiwa zaidi ya 800.
Comments