DAKTARI ANAYETUHUMIWA KUSABABISHA KIFO CHA MWANANCHI KATAVI KWA KUTOMHUDUMIA AJIFUNGUA MTOTO.
DAKTARI wa zahanati ya Kapalamsenga wilayani Mpanda,
anayetuhumiwa na wakazi wa kijiji hicho kusababisha kifo cha Bi.Ana Kilangi (49) kwa kugoma kumhudumia,
amejifungua salama.
Kwa mujibu wa Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mpanda ,Dk
Jovin Mlinda amemtaja daktari huyo kuwa ni Bi Rehema Munga aliyejifungua mtoto
mwenye uzito wa kilo tatu hospitalini hapo Jumapili iliyopita.
Siku moja kabla ya kujifungua,askari wa Jeshi la Wananchi wa
Tanzania (JWTZ) kutoka kambi ya Ikola walilazimika kuilinda nyumba yake baada
ya wananchi wenye hasira kutishia kuichoma moto .
Bi Ana Kilangi kabla ya kifo chake, alifikishwa katika
zahanati hiyo saa moja usiku kwa matibabu, lakini daktari huyo alikuwa tayari
amelala nyumbani kwake, na kutokana na hali ya ujauzito alishindwa kwenda
kumhudumia mgonjwa huyo.
Matukio ya madaktari kulalamikiwa kutotoa huduma kama
inavyostahiri kwa wagonjwa yamekuwa
yakitokea hata nje ya mkoa wa Katavi ikiwemo Mkoani Mwanza.
Comments