WAWILI WAKAMATWA WAKITUHUMIWA KUIBA MTOTO WILAYANI MPANDA
Na.Vumilia Abel
SERIKALI ya kijiji cha Ikaka kata ya Mnyagala Wilayani
Mpanda mkoani katavi kimewakamata watu wawili wanaofahamika kwa majina ya
Edefance John na Januari Kisulo wote wakazi wa kijiji cha Isengule kata ya Ikola kwa tuhuma za wizi wa mtoto mwenyeumri wa miaka
13.
Taarifa
ya kukamatwa kwa wezi hao imebainishwa juzi na Afisa mtendaji wa kijiji hicho
Bw. Bw.leonard Michael Mbogambi kupitia kikao cha hadhara kilichwashirikisha
wananchi kikilenga kujadili kusoma mapato na matumizi ya mradi wa maji.
Aidha
mtendaji huyo amesema,watu hao waliokamatwa watapelekwa katika vyombo vya
sheria na kuwa ili iwe fundisho kwa watu wenye tabia kama hiyo.
Awali
mwenyekiti wa kijiji hicho B w.Mipawa Pikipiki alisema kuwa watu hao aliwapokea
majira ya saa 4 asubuhi wakiomba hifadhi ya kulala nyumbani kwake ili kesho
yake waendelee na safari ambapo hakufahamu kuwa mtoto waliyekuwa naye siyo wao.
Kwa
upande wake askari wa sungusungu wa kijiji hicho Bw.Fredy Nkana Tung’ombe
ametoa lawama kwa wazazi juu ya tukio kwa kutomtimiza mahitaji muhimu ya mtoto.
Kwa
kwa mujibu wa askari huyo, mtoto huyo ambaye hata hawezi kujieleza amekosa
mahitaji ya msingi ikiwemo elimu,mavazi na chakula.
Kwa
upande wa watuhumiwa,wamekana kuiba mtoto ambapo wamedai kuwa walifuatwa na
mtoto huyo baada ya kumwomba awaoneshe njia ya sehemu wanakoelekea.
Kwa
upande mama mzazi wa mtoto huyo Bi.Pascharia Valentino ambaye ni mkazi wa
kijiji cha Kalofesi amesema alikuwa akiishi na watu hao kwa mwezi mmoja mpaka
sasa.
Comments