WANANCHI WILAYANI MPANDA WALIOMBA JESHI KATAVI KUONGEZA KASI YA KUZUNGUKIA MITAA KUIMARISHA USALAMA WA RAIA NA MALI ZAO.
Na.Issack Gerald-Katavi
Jeshi la Polisi Wilayani Mpanda
Mkoani Katavi,limeombwa kupita mara kwa mara katika mitaa ambayo wamekuwa
hawapiti mara kadhaa ili kuimarisha usalama na kukomesha udokozi wa mali za
raia unaoendelea.
Ombi hilo limetolewa na baadhi ya viongozi
wa serikali za mitaa pamoja na wananchi wakati wakizungumza na waandishi wa habari kuhusu udokozi wa mali za raia.
Mionogni mwa mitaa ambayo imeelezwa
kuwa Polisi hawapiti mara kwa mara ni pamoja na Mtaa wa Mpadeco na mtaa wa Kasimba
uliopo kata ya Ilembo mita chache kutoka Makao makuu ya jeshi la Polisi Mkoa wa
Katavi.
Februari 16 mwaka huu,mkaguzi
msaidizi wa Polisi Wilayani Mpanda Godfrey Ndangala akizungumza kwa niaba ya
mkuu wa Kituo cha Polisi Wilayani Mpanda,alikiri kuwepo kwa hali ya ubomoaji wa
milango,madirisha na ukataji nyavu unaosababishwa na wezi.
Matukio ya udokozi wa mali za raia umekuwepo kwa muda mrefu wilayani
Mpanda ambapo hata hivyo limepungua tofauti na ilivyokuwa kipindi cha siku
zilizopita.
Comments