RPC KATAVI ATAKA SILAHA ZISALIMISHWE
Na.Issack
Gerald-Katavi
Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi limewataka
wananchi wanaomiliki silaha kinyume cha sheria kuzisalimisha mara moja silaha
hizo katika vituo vya Polisi vilivyopo karibu na makazi yao.
Agizo hilo limetolewa na Kaimu kamanda wa
Polisi Mkoani Katavi ACP Rashid Mohamed Kwani halitositakisema kuwa hatua kali
za kisheria zitachukuliwa kwa mtu au kikundi kitakachobainika kumiliki silaha
kinyume cha sheria na taratibu za nchi.
Aidha, Kamanda walio na silaha majumbani mwao
ambazo zilikuwa zikimilikiwa kihalali na kwa sasa ndugu zao aliyekuwa akimiliki
silaha hiyo alikwishariki dunia wafuate utaratibu kwa kuzisalimisha silaha hizo
ambapo suala hili linawahusu pia wazee ambao wamefikisha umri ambao hauwaruhusu
kumiliki silaha.
Hata hivyo amesema kuwa ni kosa kisheria
wanaomiliki silaha kisheria kuziazimishwa kwa makampuni bina binafi ya ulinzi
ambapo pia amewataka kuacha tabia hiyo mara moja.
Kamanda Mohamed amesema kuwa wananchi
wanatakiwa kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi wanapoona viashiria
vyovyote vya uharifu ili vidhibitiwe kabla ya kuleta madhara.
Comments