MGONJWA ALIYEMNASA KIBAO HOSPITALI YA WILAYA YA MPANDA MKOANI KATAVI MUUGUZI ATOROKA HOSPITALINI.
Na.Issack Gerald-Katavi
Mgonjwa aliyempiga Bi.Recho Matinya
ambaye ni muuguzi wa Hospitali ya Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi wakati mgonjwa
huyo akiwa amelazwa katika Hospitali hiyo,ametoroka kutoka hospitalini hapo.
Mganga mfawidhi wa Hosptali ya Wilaya
ya Mpanda Dk.Jovin Mlinda akizungumza na P5 TANZANIA MEDIA amesema, mgonjwa huyo alitoroka siku moja baada ya
tukio la kupigwa kwa muuguzi huyo.
Tukio la kupigwa kwa muuguzi huyo
lilitokea Machi 08 mwaka huu katika wodi ya wagonjwa baada ya mgonjwa huyo kutakiwa
kulala pamoja na mgonjwa mwingine
kutokana na uhaba wa vitanda katika hospitali hiyo.
Inasemekana kuwa huenda mgonjwa huyo
akawa ametoroshwa na ndugu zake kwa wakati ambao ndugu huingia kuwaona wagonjwa
wao kwa Dk.Jovin Mlinda amesema kuwa hakuna taarifa zinazoonesha kuwa kuna
daktari alimuruhusu mgonjwa huyo kuondoka.
Mbali
na tukio hilo kutokea mkoani Katavi,Machi 8 mwaka huu,madaktari
katika Hospitali ya Butimba wilayani
Nyamagana Mkoani Mwanza, nao waligoma kutoa huduma kwa zaidi ya saa sita wakidai
kunyanyaswa na kutishwa na watu
wanaofika hospitalini hapo kupata huduma.
Comments