KUKMBUKUMBU YA MIAKA 32 YA KIFO CHA WAZIRI MKUU MZALENDO HAYATI EDWARD MORINGE SOKOINE
(Na.Issack
Gerald-P5 TANZANIA MEDIA)
Hayati
Sokoine alizaliwa mnamo mwaka 1/8/1938 katika wilaya ya MAASAI LAND ambayo kwa
sasa inafahamika kama wilaya ya Monduli iliyopo mkoani Arusha.
Waziri Mkuu wa awamu ya 3 na 5 wa Tanzania |
Hayati
Sokoine alipata elimu yake ya msingi Monduli,akafaulu kujiunga na shule ya
sekondari Umbwe,hii ilikuwa ni kuanzia mwaka 1948 mpaka 1958.
Alipomaliza
hapo alijiunga rasmi na chama cha TANU 1961 wakati taifa letu tukufu Tanganyika
likipata uhuru wake.
Kisha
alipata nafasi ya kwenda nchini Ujerumani mwaka 1962 mpaka 1963 kusomea mambo
ya uongozi na utawala na aliporudi akateuliwa kuwa afisa mtendaji wilaya ya
Maasai Land kama nilivyokwambia kwa sasa ni Monduli nah ii ikiwa ni kutokana na
ufanyakazi wake uliotukuka wilayani Monduli.
Wananchi
hawakuwa na budi kumchagua,wakamchagua kuwa mwakilishi wao bungeni yaani mbunge
wa Monduli na ufanisi wake kiutendaji ulionekana machoni mwa watendaji wakuu wa
serikali.
Hayati baba
wa taifa Julius Kambarage Nyerere na hatimaye akamchaguwa kuwa Naibu wa wizara
ya mawasiliano na Usafiri hii ilikuwa mwaka 1967.
Haikuishia
hapo,nyota ya kiuongozi ilizidi kumwangazia hayati Sokoine ambapo mwaka 1972
aliteuliwa kuwa waziri wa Usalama na hatimaye mwaka 1977 aliteuliwa rasmi kuwa
waziri Mkuu wa iliyokuwa serikali ya Tanganyika,na Muungano wa Tanzania kipindi
hicho.
Kama
utakumbuka mwaka 1977 ni mwaka ambao katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
tunayotumia kwa sasa ilitungwa kwati huo ikiwa chini ya mwamvuli wa chama
kimoja kwani mfumo wa vyama vingi vya siasa ulianzishwa miaka 7 baadaye yaani
mwaka 1992 na kuwa na uchaguzi wa wa kwanza wa vyama vingi vya saiasa mwaka
1995 uongozi wa mfumo huo ukianzia kwa Rais wetu wa awamu ya Tatu Benjamini
Willium Mkapa.
Hayati sokoine alikuwa hasa aliependa siasa za ujamaa na hata kupelekea kumwomba baba wa taifa ruhusa ya kusimama kwa mda kama waziri mkuu ili aende kusomea zaidi mambo ya ujamaa nchi za nje hiyo ikiwa ni mwaka 1981,1983 ambapo baadaye alirudi kuendelea kama waziri mkuu wa Tanzania mpaka siku ya tarehe 12/4/1984 alipopata ajali mbaya ya kugongwa na gari lililokuwa likiendeshwa na mkimbizi wa kisiasa kutoka nchini Afrika kusini aliyejulikana zaidi kwa jina la Dube,eneo la Wami Dakawa kwa sasa eneo hilo lilikwishabatizwa jina linguine na kuitwa Wami Sokoine mkoani Mororgoro.
Hayati sokoine alikuwa hasa aliependa siasa za ujamaa na hata kupelekea kumwomba baba wa taifa ruhusa ya kusimama kwa mda kama waziri mkuu ili aende kusomea zaidi mambo ya ujamaa nchi za nje hiyo ikiwa ni mwaka 1981,1983 ambapo baadaye alirudi kuendelea kama waziri mkuu wa Tanzania mpaka siku ya tarehe 12/4/1984 alipopata ajali mbaya ya kugongwa na gari lililokuwa likiendeshwa na mkimbizi wa kisiasa kutoka nchini Afrika kusini aliyejulikana zaidi kwa jina la Dube,eneo la Wami Dakawa kwa sasa eneo hilo lilikwishabatizwa jina linguine na kuitwa Wami Sokoine mkoani Mororgoro.
Ajali hiyo ilipelekea
mauti yake palepale,kifo ambacho mpaka leo kinaacha maswali mengi na kwa bahati
mbaya hakuna hata mwandishi mmoja aliefanya mahojiano na bwana Dube ambaye kwa
sasa yupo nchini Afrika kusini anakula bata baada ya kuachiwa huru.
Itakumbukwa
kwamba karibia viongozi wakubwa wote wa serikali waliondoka mjini Dodoma kwa
ndege mara baada ya kikao cha NEC,Isipokuwa hayati Sokoine ,yeye alisema wazi
ni muumini wa sera ya kilimo ni uti wa mgongo wa taifa,hivyo alipendekeza
kusafiri kwa njia ya barabara ili ajionee Mashamba makubwa na maendeleo ya
kilimo kwa ujumla,
Miongoni
mwa maneno aliyoyasema mwaka 1984 mwezi April kabla ya kufariki dunia ambayo yatakumbukwa na watnzania daima ni haya
hapa.
"Ole wao wale wanaotumia nafasi zao za
umma na serikali,kuiba,kuhujumu uchumi,kupokea rushwa,maana salama yao ni kudra
za Mwenyezi Mungu labda nisiwajue"
Hayati Sokoine aliongoza vipindi viwili tofauti kuanzia 13 Februari 1977 hadi 7 Novemba 1980 CCM na baadaye tena 24 Februari 1983 hadi 12 Aprili 1984 CCM.
Hayati Sokoine aliongoza vipindi viwili tofauti kuanzia 13 Februari 1977 hadi 7 Novemba 1980 CCM na baadaye tena 24 Februari 1983 hadi 12 Aprili 1984 CCM.
Orodha
ya Viongozi wa Serikali ya Tanzania
Waziri
Kiongozi wa Tanganyika
|
|||
Jina
|
Amechukua Ofisi
|
Ameondoka Ofisini
|
Chama
|
2 Septemba 1960
|
1 Mei 1961
|
||
Mawaziri
Wakuu wa Tanganyika
|
|||
1 Mei 1961
|
22 Januari 1962
|
||
22 Januari 1962
|
9 Desemba 1962
|
||
Nafasi
Zilizoondolewa Tangu (9 Desemba 1962-17 Februari 1972)
|
|||
Mawaziri
Wakuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
|
|||
17 Februari 1972
|
13 Februari 1977
|
||
13 Februari 1977
|
7 Novemba 1980
|
||
7 Novemba 1980
|
24 Februari 1983
|
||
24 Februari 1983
|
12 Aprili 1984
|
||
24 Aprili 1984
|
5 Novemba 1985
|
||
5 Novemba 1985
|
9 Novemba 1990
|
||
9 Novemba 1990
|
7 Desemba 1994
|
||
7 Desemba 1994
|
28 Novemba 1995
|
||
28 Novemba 1995
|
30 Desemba 2005
|
||
30 Desemba 2005
|
7 Februari 2008
|
||
9 Februari 2008
|
20 Novemba 2015
|
Kassim
Majliwa 20 Nov,2016 hadi sasa CCM
Comments