JESHI LA ZIMAMOTO WALALAMIKIWA NA WAKAZI KATAVI KWA KUWAPA VITISHO WENYE MFUMO WA UTAPELI
NA.Issack Gerald-Katavi
Wafanyabiasha
wa soko la Buzogwe wamelalamikia hatua ya kikosi cha zima moto Manispaa ya
Mpanda mkoani wa Katavi kwa kuwatoza
kodi ambayo haijulikani inakopelekwa pamoja na kutoelimishwa juu ya michango
hiyo.
Mwonekano wa gari la zimamoto (PICHA NA Issack Gerald) |
Wakizungumza
katika mkutano ulioitishwa na uongozi wa soko hilo,wamesema kikosi hicho kinawatoza kodi ya Shilingi Elfu Arobaini.
Wamesema
kuwa askari hao wamekuwa wakiwapa vitisho vya kuwapeleka mahakamani na kuonesha
ubaguzi kwa baadhi ya wafanyabiahara kuhusu kulipa kodi hiyo huku wengine
wakiwa hawalipi kabisa.
Kwa
upande wake mwenyekiti wa soko hilo Bw. Ramadhani Karata amekiri askari hao
kuwatisha wafanyabiashara na kuwakuzia faini kwa wale ambao hawajalipa licha ya
kuwa hawana elimu kuhusu michango hiyo.
Akijibu
malalamiko hayo, Mkaguzi Mkuu wa jeshi la zimamoto na uokoaji Mkoa wa katavi Kamanda
Edward Kakwale amesema, kodi hiyo ni ya serikali nzima inayojulikana kama kodi
ya ukaguzi zimamoto ambayo hutozwa kwa wafanyabiasha walio na maduka
yanayotambulika kisheria.
Aidha
Kamanda Kakwale amesema kodi hiyo hulipwa
mara moja kwa mwaka mzima na hupelekwa katika mfuko wa serikali kwa
ajili ya majukumu mengine ya kiserikali.
Comments