WABUNGE KATAVI WACHACHAMALIA MAJI,UMEME BARABARA
Na.Issack
Gerald-Bungeni Dodoma (Kuhusu Katavi).
SERIKALI
imeanza mikakati ya kukamilisha miradi ya maji
ili wananchi wapate maji kama ilivyo kusudiwa.
Hayo
yamejili leo bungeni mjini Dodoma baada ya mbunge wa mpanda vijijin Bw. Suleiman
Moshi Kakoso na mbunge wa jimbo la Ngara Bw. Alex Raphael Gashaza kutaka
kufahamu mikakati ya serikali kwa wananchi katika kuwaletea huduma ya maji.
Akijibu
maswali yaliyoulizwa na wabunge hao Naibu Waziri wa Waziri wa Maji na Umwagiliaji Gerson Lwenge waziri
wa maji na umwagiliaji mhandisi Gerson Lwenge amesema serikali imeanza kuchukua
hatua ya kuhakikisha huduma hiyo inamfikia kila mwananchi.
Mhandisi
Lwenge amesema miradi ya umwagiliaji
mwaka 2015/2016 imetengewa fedha kiasi cha shilingi bilioni 53 katika
kuendeleza sekta ya umwagiliaji ambayo inasimamiwa na tume ya umwagiliaji.
Wakati
huo huo mbunge wa jimbo la Kavuu Mkoani Katavi Bi. Pudensiana Kikwembe amehoji serikali
ina mpango gani wa kuwaletea wananchi wa eneo hilo nishati ya umeme ambapo akijibu
swali hilo naibu waziri wa nishati na madini Bw. Menod kalemani amesema
wanaendelea na ukarabati wa miundombinu ili wananchi wote wapate nishati hiyo.
Comments