MWANAFUNZI SHULE YA MSINGI AFA MAJI MPANDA
Na.Issack Gerald-Mpanda
Mwanafunzi
shule ya msingi Kashato aliyejulikana kwa jina la Julius Justin Albano(12) mwanafunzi
wa darasa la sita shule ya msingi Kashato amekufa maji akiwa anavua samaki
katika mto Mpanda maeneo ya Kigamboni.
Kamanda
wa Polisi Mkoani Katavi Dhahiri Kidavashari amesema kuwa tukio hilo limetokea mnamo
tarehe 03/02/2016 majira ya saa 4 asubuhi katika maeneo ya Kigamboni kata ya
Nsemulwa Tarafa ya Kashaulili Wilayani Mpanda Mkoani Katavi.
Kamanda kidavashari amesema kuwa,tarehe
02/02/2015 majira ya saa 12:00 mama mzazi wa marehemu aliyejulikana kwa jina la
Prisca selemani (35) mkazi wa Kigamboni alimwagiza dukani kwenda kununua sabuni
ambapo baada ya kumwagiza,yeye alielekea msibani huko maeneo ya Nsemulwa na ilipofika
majira ya saa 06:00 mchana alirudi nyumbani na kukuta marehemu hayupo, ndipo
alipoanza kumtafuta bila mafanikio.
Ilipofika
tarehe 03/02/2016 majira ya asubuhi alipata taarifa kuwa marehemu alionekana
maeneo ya pembezoni mwa mto Mpanda akiwa na watoto wenzake wanavua samaki.
Baada
ya kupata taarifa hizo walianza kumtafuta maeneo hayo na walifanikiwa kuukuta
mwili wa marehemu ukiwa umezama chini ya maji katika mto Mpanda maeneo ya
kigamboni.
Mwili
wa marehemu umekabidhiwa kwa ndugu zake kwa ajili ya mazishi baada ya uchunguzi
wa kitabibu kwani hapakuwa na shaka yoyote juu ya kifo hicho.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Katavi ametoa wito kwa jamii kuendelea kuwaelimisha watoto
kuacha tabia ya kwenda kucheza,kuogelea au kuvua samaki kwenye mito, madimbwi
ya maji hasa wakati huu wa msimu wa mvua ili kuweza kujiepusha na matukio ya
namna hii yasitokee ndani ya jamii.
Comments