ASASI ZA BINAFSI ZA KIRAIA NA SERIKALI ZAAGIZWA KUELIMISHA JAMII MASUALA YA SHERIA KATAVI,RAIS MAGUFULI NAYE ATOA AGIZO KALI DAR,MAHAKAMA YA MAFISADI KUJENGWA MWAKA HUU
Na.Issack
Gerald-Katavi
Asasi za kiraia na zile za serikali zikiwemo
vyombo vya habari, wanaharakati wa haki za binadamu wametakiwa kushirikiana kwa
pamoja kuelimisha jamii juu ya kanuni zinazotumika kushughulikia kudai haki za
madai na jinai kwa mjibu wa kanuni na sheria hapa nchini.
Wito huo umetolewa na Mganga Mkuu wa
Mkoa Dk Yahya Hussein kwa niaba ya Mkuu
wa Mkoa wa Katavi katika maadhimisho ya siku ya sheria duniani ambayo katika
Mkoa wa Katavi maadhimisho haya yamefanyika katika viwanja vya mahakama ya Wilaya
ya Mpanda.
Kwa upande wake Farhat Seif wakili wa
Serikali Mfawidhi Mkoani Katavi pamoja na kuzungumza masuala mbalimbali amesema
kuwa watumishi wa mahakama na wadau wengine wa sheria wanatakiwa kuzingatia maadili ya kazi yao ikiwemo
kutojihusisha na vitendo vya rushwa ili kuepuka wananchi kujichukulia sheria
mikononi kutokana na wananchi kukosa imani na vyombo vya maauzi.
Naye mwenyekiti wa Taasisi ya isiyo
ya kiserikali ya Tanganyika Law Sciety Mh.Simon Buchur ambaye pia ni mwakilishi
wa Takukuru Taasisi ya kupambana na rushwa Mkoani Katavi amesema kuwa manung’uniko
ya wananchi kwa vyombo vya mahakama vitakwisha ikiwa mwananchi atatendewa haki
mahakamani ipasavyo bila kucheleweshwa pamoja na kupatiwa nakala ya kesi
inayomhusu mhusika ili kama ni kukata rufaa kwa mjibu wa sheria afanye kama inavyotakiwa.
Maadhimisho haya pia yamehudhuriwa na
Hakimu mkazi Mfawidhi Wilaya ya Mpanda Chiganga Tengwa ambaye pia ndiye anayekaimu
mahakama ya hakimu Mkazi ya Mkoa wa Katavi,Wakili Adolf Mishanga mwakilishi wa Shirika la Wwakimbizi la umoja
wa mataifa la UNHCR Mishamo,watumishi mbalimbali wa mahakama,wadau mbalimbali
wa heria na wananchi.
Hata hivyo licha ya kuwa baadhi ya
wananchi walio wengi wameonesha kutotambua maana ya siku ya sheria
duniani,baadhi ya waliohudhuria sherehe hizi wameeleza kujifunza mengi ambayo
yatakuwa msaada mkubwa katika maisha yao ya kila siku ikiwemo kuzingatia msemo
kuwa ‘’Kutofahamu sheria siyo kinga ya kupatiwa adhabu’’
Wakati hayo yakiwa yamejiri Mkoani
Katavi,Jijini Dar es Salaa,mgeni rasmi wa maadhimisho hayo Rais Dk.John Pombe
Magufuli ameviagiza vyombo vyote
vinahusika katika kutoa haki kuhakikisha vinatoa haki kwa wakati na kwa wale
wote wanaoharibu sifa za vyombo hivyo wachuliwe hatua ikiwa ni kiiashirio cha
kuanza mwaka wa mahakama hapa nchini.
Aidha Rais ameagiza kuharakishwa
kuundwa kwa mahakama ya kushughulikia mafisadi na watu wanaojihusisha na rushwa
kwani hatua hiyo ni muhimu kwa maendeleo ya taifa.
Kwa upande wake Jaji Mkuu
wa Tanzania Mhe.Mohamed Chande Othman amesema
kuwa wapo katika mchakato ili kuhakikisha mahakama hiyo inafanya kazi kwa mwaka
huu wa 2016.
Kauli mbiu katika maadhimisho ya
mwaka huu ni ‘’UTOAJI WA HAKI
INAYOMLENGA MTEJA,WAJIBU WA MAHAKAMA NA WADAU.
Nchini Tanzania Maadhimisho ya siku
ya sheria yalianzishwa mwaka 1996 ambapo kitaifa mwaka huu yameadhimishwa
Jijini Dar es Salaam na Mgeni Rasmi akiwa ni Rais wa Tanzania John Pombe
Magufuli kwa uongozaji mkuu wa Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe.Mohamed Chande
Othman.
Comments