MATUKIO YA WIKI KATAVI NA TANZANIA KWA UJUMLA FEBRUARI 01—06 ,2016



Na.Issack Gerald-Katavi
Monday, 1 February 2016
Posted By:Issack Gerald | At:Monday, February 01, 2016


Na.Issack Gerald-Mpanda
JAMII wilayani Mpanda Mkoani Katavi  imetakiwa kutambua haki ya elimu kwa watoto wenye ulemavu kwa kuwaandikisha katika shule zinazotoa elimu maalumu kwa watoto walemavu.

Akizungumza na P5 TANZANIA MEDIA  Afisa elimu kitengo cha vifaa na takwimu wa halmashauri ya wilaya ya mpanda Bw. Amos Mwasa amesema elimu ni haki ya kila mtu, hivyo wazazi wenye watoto wenye ulemavu watambue haki ya watoto wao ya kupata elimu stahiki.
Aidha Bw. Mwasa amesema baadhi wa wazazi wamekuwa wakiwaficha watoto wao, pasipo kuwapeleka shule na kuwanyima haki ya kupata elimu.
Amesema mwitikio wa kuandikisha watoto wenye ulemavu katika shule ya Kakora bado ni mdogo kwani mpaka sasa wameandikishwa wanafunzi wanane tu.     

 Tuesday, 2 February 2016

Posted By:Issack Gerald | At:Tuesday, February 02, 2016

Na.Issack Gerald-Mpanda
ZAIDI ya walimu watatu wamekuwa wakifundisha wanafunzi wenye ulemavu katika shule ya msingi Azimio katika darasa moja na ubao mmoja kwa darasa la kwanza hadi la saba kwa miaka saba sasa.

Hayo yamebainishwa na walimu wa shule ya Msingi Azimio akiwemo mwalimu mkuu wa Shule hiyo Mwl.Beno Mahema ambapo imebainika kuwa miongoni mwa chanzo cha hali hiyo ni Mkandarasi kufunga madarasa akishinikiza kulipwa zaidi ya milioni 28 anazodai.
Kaimu Mkurugenzi Manispaa ya Mpanda Bw.Lauteri Kanoni amekiri kuwepo hali hiyo na amesema kuwa Alhamisi ya Februari 4 mwaka huu wanatarajia kufanya mazungumzo baina ya uongozi wa Manispaa na Mkandarasi ili pesa inayodaiwa Manispaa zilipwe na madarasa yaruhusiwe kutumiwa na wanafunzi.
Mpaka sasa kuna Jumla ya Wanafunzi wenye ulemavu 18,walimu 4 ambapo hata hivyo katika mpango wa Rais wa elimu bure wametengewa shilingi laki tatu kwa ajiri ya chakula.
Kwa upande wake Mkandarasai wa Kampuni ya Mwandoya Investment Bw.Paul Luguyashi ameendelea kusemakuwa hataruhusu madarasa yatumiwe na wanafunzi mpaka atakapopewa malipo yake ya zaidi ya Shilingi milioni 28 kwa sasa.
Kwa mjibu wa Mkataba wa makubaliano,mkandarasi huyu ilitakiwa alipwe shilingi milioni 32 kama sehemu ya mkataba wote baada ya kukamilisha ujenzi wa majengo mwezi Aprili mwaka 2014 baada ya kupewa tenda hiyo mwaka 2013.
Kwa hiyo kutokana na malimbikizo ya deni la Shilingi milioni 5 kutoka mwaka 2014,ilizidi kuongezeka pamoja na riba yake kutoka milioni 5 hadi kufikia zaidi ya Shilingi milioni 28 anazodai hadi sasa.
Hata hivyo Bw.Lunguya ameendelea kusisitiza kuwa katu hatofungua madarasa hayo ikiwa hatalipwa pesa yake anayodai.
Katika hatua nyingine,wazazi wenye watoto wenye ulemavu Mkoani Katavi wametakiwa kuwapeleka shuleni ili wakapate haki yao ya elimu kama walivyo watoto ambao siyo walemavu.
Wanafunzi walemavu walipo katika shule ya msingi Azimio ni wasioona,wasiosikia,wenye ulemavu wa akili na viungo ambpo kwa Mkoa wa Katavi zipo shule karibu tano zenye watoto wenye mahitaji maalumu ambapo kwa Manispaa ya Mpanda mbali na Azimio shuleni nyingine ni Shule ya Msingi Nyerere yenye wanafunzi wenye mtindio wa ubongo.
Hata hivyo wanafunzi wote wawili waliofanya mtihani mwaka 2015 walifaulu kwa daraja B na C na kuwa miongoni mwa wanafunzi waliosababisha Manispaa ya Mpanda kuongoza kwa miaka miwili mfululizo kitaifa katika matokeo ya darasa la saba.
Mshirikishe mwenzako kasha toa maoni yako mdau wangu kupitia hapahapa P5 TANZANIA MEDIA au geraldissack@gmail.com

 Tuesday, 2 February 2016

Posted By:Issack Gerald | At:Tuesday, February 02, 2016

Na.Issack Gerald-Mpanda
Mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Gidison Visent(32), mkazi wa Katuma aliuawa kwa kuchomwa na kisu kifuani na Mohamed Muna (59) mratibu elimu Kata mkazi wa Katuma.

Kamanda wa Polisi Mkoani Katavi Dhairi Kidavashairi amesema kuwa tukio hilo lilitokea mnamo tarehe 27.01.2016 majira ya saa mbili na nusu usiku katika Kitongoji cha Mashineni kijiji na Kata ya ya Katuma Tarafa ya Mwese Wilayani Mpanda Mkoani Katavi.
 Kamanda Kidavashari,amesema kuwa mtuhumiwa alimkuta marehemu akiwa ndani ya nyumba yake huku akiwa anafanya mapenzi na mke wake aliyejulikana kwa jina la Ester Kasansa Chuki(36) mkazi wa Katuma.
Bw.Muna alipogonga mlango,marehemu alitoka nje na kuanza kupambana naye ambapo mtuhumiwa ambaye ni Muna alimchoma kisu kifuani na kukimbia.
Chanzo cha tukio hili ni wivu wa kimapenzi.
Hata hivyo Jeshi la Polisi linamshikilia mtuhumiwa kwa mahojiano zaidi na anatarajiwa kufikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika kujibu tuhuma inayomkabili.

 Wednesday, 3 February 2016

Posted By:Issack Gerald | At:Wednesday, February 03, 2016

Na.Issack Gerald-Mpanda
Mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Zuhura Salum(34), mkazi wa Majengo alijeruliwa kwa kuchomwa na kisu kwenye titi la kulia na Iddy Saleh(24), mkazi wa majengo na kumsababishia maumivu makali.

Kamanda wa Polisi Mkoani Katavi Dhahiri Kidavashari amesema kuwa tukio hilo limetokea mnamo tarehe 29.01.2016 majira ya saa tatu asubuhi katika maeneo ya Majengo “B” Kata na Tarafa ya Kashaulili Wilayani Mpanda Mkoani Katavi.
Kamanda Kidavashari amesema kuwa mhanga na mtuhumiwa walikuwa wamelala kwenye nyumba ya kulala wageni inayojulikana kwa jina la maridadi ndipo mtuhumiwa aliamka na kumvizi akiwa usingizini na kumchoma na kisu kwenye titi la kulia.
Chanzo cha tukio hili bado kujulikana ambapo hata hivyo mtuhumiwa anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa mahojiano zaidi na anatarajiwa kufikishwa mahakmani kujibu tuhuma inayomkabili.
Wakati huo huo katika tukio lingine mtu mwingine aliyejulikana kwa jina la Kalekwa Otto(28), mkazi wa kamukuswe alijeruliwa kwa kukatwa na panga mkono wa kulia na kwa kushoto na Manyara Otto na kumsababishia majeraha
Aidha Kamanda Kidavashari amesema kuwa tukio hili limetokea juzi 01.02.2016 majira ya saa moja kijiji cha  kamkuswe kata na tarafa ya mwese wilayani mpanda mkoani katavi.
Amesema kuwa mtuhumiwa na mhanga ni mtu na kaka yake ambapo Siku ya tukio wakiwa kwenye kilabu cha pombe huku wakiendelea kunywa ndipo ulipozuka ugomvi kati ya ndugu hawa wawili na Manyara Otto alipomkata kwa panga na mara baada ya kutenda kosa hilo alitokomea kusikojulikana.
Hata hivyo Chanzo cha tukio hili ni ugomvi wa kifamilia kati ya ndugu hawa wawili na Jeshi la Polisi linaendelea kumsaka alipokimbilia mtuhumiwa ili kujibu tuhuma inayomkabili.   
Wakati huo huo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi amewataka wananchi kujenga mazoea ya kuwasilisha matatizo yao katika mamlaka za kisheria ili yaweze kupatiwa ufumbuzi na badala yake waachane na tabia ya kujichukulia sheria mikononi kwa kufanya vitendo viovu vinavyopelekea matatizo makubwa ndani ya familia.
Wednesday, 3 February 2016
Posted By:Issack Gerald | At:Wednesday, February 03, 2016

Na.Agness Mnubi-Nsimbo.
HALMASHAURI ya Wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi imeidhinisha kiasi cha shilingi billion 26,043,182,000 (Bilioni 26 milioni 43 na mia moja themanini na mbili elfu)  kwa ajili ya kutekeleza MIRADI mbalimbali iliyopangwa kufanyika katika Halmashauri hiyo kwa mwaka wa fedha 2016/2017.
Fedha hizo zimeidhinishwa  na Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo katika kikao cha bajeti ya mwaka wa fedha 206-2017 kilichofanyika leo katika ukumbi wa halmashauri hiyo.
Akisoma Bajeti hiyo mkuu wa idara ya mipango takwimu na ufuatiliaji Fredinand Filimbi amesema bajeti iliyotengwa imeandaliwa kwa  imezingatia sera na miongozo mbalimbali ya kitaifa.
Aidha bw. Filimbi amefafanua mchanganuo wa fedha hizo utatumika katika masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na mishahara,miradi ya maendeleo, na matumizi ya kawaida.
Amesema kiwango cha mapato ya ndani kwa mwaka wa fedha 2016-2017 kimeongezeka kwa asilimia 12 na kutaja baadhi ya vyanzo vya ukusanyaji wa mapato hayo ikiwemo ushuru wa mifugo,magulio,nyama na vyombo vya uvuvi.
Aidha akifunga kikao hicho Mwenyekiti wa baraza la madiwani Rafael Kalinga ambaye ni diwani wa kata ya Machimboni amewataka madiwani na watumishi kuendelea kushirikiana ili kufikia malengo ya bajeti hiyo pamoja na kusimamia ukusanyaji wa mapato ,pia amewataka wakuu wa idara  kuhakikisha wanatekeleza miradi ya nyuma ambayo ilitengewa fedha.

 Wednesday, 3 February 2016

Posted By:Issack Gerald | At:Wednesday, February 03, 2016

Na.Issack Gerald-Dodoma
Mbunge wa Mpanda Mjini Mheshimiwa Sebastian Kapufi ameiomba Serikali kuweka nguvu yake katika ujenzi wa chuo kikuu cha kilimo kinachotarajiwa Mjini Mpanda kwa ajiri ya Kuongeza ajira kwa wakazi wa Mkoa wa Katavi na Mioko mingine.
Mheshimiwa Sebastian Kapufi ameuliza swali hilo akiwa bungeni Mjini Dodoma ambapoa akijibu swali hilo,Naibu waziri wa Elimu, sayansi,teknolojia na ufundi Injinia Stela Martin Manyanya amesemakuwa tayari tume ya vyuo viku ilikwishatoa hati kwa ajiri ya ujenzi wa chuo kikuu hicho kinachomilikiwa na  Manispaa ya Mpanda ambapo amesemakuwa serikali itaendelea kutoa ushauri wa kitaalamu nakiufundi ili kukamilisha ujenzi wa Chuo kikuu cha kilimo cha Katavi.
Aidha Serikali kupitia wizara ya Elimu, sayansi,teknolojia na ufundi imeshauri Manispaaya Mpanda kushirikisha balaza la madiwani ili kuondoa hali ya sintofahamu juu ya ujenzi wa chuo hicho ambacho kama kingekuwa kinaendelea kujengwa mpaka sasa kingekuwa kimekwishapata Doala za kimarekani Milioni 2.5 kwa udhamini wa benki ya biashara ya AFRICAN TRADING INSURANCE AGENCE.
Hata hivyo Injini Stela Manyanya amesema Manispaa ilikwishapata eneo la ekari 500 kwa ajiri ya ujenzi wa ujenzi wa chuo hicho.
Kwa upande wake Waziri wa elimu sayansi,teknolojia na ufundi Profesa Joyce Ndalichako amesema kuwa chuo hiki kinajengwa na Manispaa baada ya kuomba wizarani juu ya ujenzi wa chio hicho.
Uamuzi wa Ujenzi wa Chuo kikuu cha Kilimo ulitolewa mwaka feb 11,2011 kupitia vikao vya kisheria vya Halmshauri ya Manispaa ya Mpanda kwa kuzingatia sheria ya seriklai za mitaa serikali ya mtaa no.8 ya 1982(5) kifungu  53 na 54 1(a) na (b) na 2 (b) na (c).
Tume ya vyuo vikuu ilitoa hati ya usajiri wa awali ya uanzishwaji wa chuo hiki  kwa barua yenye kumbukumbu no.TCU/A/40/1A/V34 YA 31/01/2012 ambapo Manispaa ya Mpanda ilikuwa kikishirikiana wadau mbalimbali kikiwemo chuo cha kilimo cha Uingereza kukamilisha masharti ya uanzishwaji wa chuo hiki.

 Wednesday, 3 February 2016

Posted By:Issack Gerald | At:Wednesday, February 03, 2016

Na.Issack Gerald-Dodoma kuhusu (Rukwa)
SERIKALI imesema mwaka wa fedha 2015/2016 ilitenga Shillingi million 300 kwa ajili matengenezo na ujenzi wa Barabara ya Kitosi- Wampembe katika Wilaya ya Nkasi Mkoa wa Rukwa kupitia Wakala wa Barabara (TANROADS) ili kufanya Barabara hiyo iweze kupitika katika kipindi chote cha mwaka.
Serikali imetoa jibu hilo wakati wa swali la Mheshimiwa Mbunge Desdelius John Mipata Mbunge wa Nkasi Kusini ambaye ametaka kufahamu  mikakati ya serikali ya kilio cha  wananchi wanaopata shida kwa Barabara hizo kutopitika katika kipindi chote cha mwaka.
Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani amesema Serikali kupitia Wizara yake imesikia kilio cha wananchi wa Wilaya ya Nkasi na inaendelea kutoa fedha za matengenezo ya Barabara ya Kitosi-wampembe.
Ukarabati wa barabara ya Kitosi-Wampembe yenye urefu wa kilomita 67 na Barabara ya Nkana –kala yenye urefu wa kilometa 68 uko chini ya Mfuko wa Barabara ikisimamiwa na Wakala wa Barabara (TANROADS) na Barabara zote ziko chini ya Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi.
Thursday, 4 February 2016
Posted By:Issack Gerald | At:Thursday, February 04, 2016

Na.Issack Gerald-Mpanda

Mwanafunzi shule ya msingi Kashato aliyejulikana kwa jina la Julius Justin Albano(12) mwanafunzi wa darasa la sita shule ya msingi Kashato amekufa maji akiwa anavua samaki katika mto Mpanda maeneo ya Kigamboni.

Kamanda wa Polisi Mkoani Katavi Dhahiri Kidavashari amesema kuwa tukio hilo limetokea mnamo tarehe 03/02/2016 majira ya saa 4 asubuhi katika maeneo ya Kigamboni kata ya Nsemulwa Tarafa ya Kashaulili Wilayani Mpanda Mkoani Katavi.
 Kamanda kidavashari amesema kuwa,tarehe 02/02/2015 majira ya saa 12:00 mama mzazi wa marehemu aliyejulikana kwa jina la Prisca selemani (35) mkazi wa Kigamboni alimwagiza dukani kwenda kununua sabuni ambapo baada ya kumwagiza,yeye alielekea msibani huko maeneo ya Nsemulwa na ilipofika majira ya saa 06:00 mchana alirudi nyumbani na kukuta marehemu hayupo, ndipo alipoanza kumtafuta bila mafanikio.
Ilipofika tarehe 03/02/2016 majira ya asubuhi alipata taarifa kuwa marehemu alionekana maeneo ya pembezoni mwa mto Mpanda akiwa na watoto wenzake wanavua samaki.
Baada ya kupata taarifa hizo walianza kumtafuta maeneo hayo na walifanikiwa kuukuta mwili wa marehemu ukiwa umezama chini ya maji katika mto Mpanda maeneo ya kigamboni.
Mwili wa marehemu umekabidhiwa kwa ndugu zake kwa ajili ya mazishi baada ya uchunguzi wa kitabibu kwani hapakuwa na shaka yoyote juu ya kifo hicho.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi ametoa wito kwa jamii kuendelea kuwaelimisha watoto kuacha tabia ya kwenda kucheza,kuogelea au kuvua samaki kwenye mito, madimbwi ya maji hasa wakati huu wa msimu wa mvua ili kuweza kujiepusha na matukio ya namna hii yasitokee ndani ya jamii. 

 Thursday, 4 February 2016

Posted By:Issack Gerald | At:Thursday, February 04, 2016

Na.Issack Gerald-Bungeni Dodoma (Kuhusu Katavi).
SERIKALI imeanza mikakati ya kukamilisha miradi ya maji  ili wananchi wapate maji kama ilivyo kusudiwa.

Hayo yamejili leo bungeni mjini Dodoma baada ya mbunge wa mpanda vijijin Bw. Suleiman Moshi Kakoso na mbunge wa jimbo la Ngara Bw. Alex Raphael Gashaza kutaka kufahamu mikakati ya serikali kwa wananchi katika kuwaletea huduma ya maji.
Akijibu maswali yaliyoulizwa na wabunge hao Naibu Waziri wa Waziri wa Maji na Umwagiliaji  Gerson Lwenge waziri wa maji na umwagiliaji mhandisi Gerson Lwenge amesema serikali imeanza kuchukua hatua ya kuhakikisha huduma hiyo inamfikia kila mwananchi.
Mhandisi Lwenge  amesema miradi ya umwagiliaji mwaka 2015/2016 imetengewa fedha kiasi cha shilingi bilioni 53 katika kuendeleza sekta ya umwagiliaji ambayo inasimamiwa na tume ya umwagiliaji.
Wakati huo huo mbunge wa jimbo la Kavuu Mkoani Katavi Bi. Pudensiana Kikwembe amehoji serikali ina mpango gani wa kuwaletea wananchi wa eneo hilo nishati ya umeme ambapo akijibu swali hilo naibu waziri wa nishati na madini Bw. Menod kalemani amesema wanaendelea na ukarabati wa miundombinu ili wananchi wote wapate nishati hiyo.
Thursday, 4 February 2016
Posted By:Issack Gerald | At:Thursday, February 04, 2016

Na.Issack Gerald-Katavi
Asasi za kiraia na zile za serikali zikiwemo vyombo vya habari, wanaharakati wa haki za binadamu wametakiwa kushirikiana kwa pamoja kuelimisha jamii juu ya kanuni zinazotumika kushughulikia kudai haki za madai na jinai kwa mjibu wa kanuni na sheria hapa nchini.
Wito huo umetolewa na Mganga Mkuu wa Mkoa  Dk Yahya Hussein kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi katika maadhimisho ya siku ya sheria duniani ambayo katika Mkoa wa Katavi maadhimisho haya yamefanyika katika viwanja vya mahakama ya Wilaya ya Mpanda.
Kwa upande wake Farhat Seif wakili wa Serikali Mfawidhi Mkoani Katavi pamoja na kuzungumza masuala mbalimbali amesema kuwa watumishi wa mahakama na wadau wengine wa sheria  wanatakiwa kuzingatia maadili ya kazi yao ikiwemo kutojihusisha na vitendo vya rushwa ili kuepuka wananchi kujichukulia sheria mikononi kutokana na wananchi kukosa imani na vyombo vya maauzi.
Naye mwenyekiti wa Taasisi ya isiyo ya kiserikali ya Tanganyika Law Sciety Mh.Simon Buchur ambaye pia ni mwakilishi wa Takukuru Taasisi ya kupambana na rushwa Mkoani Katavi amesema kuwa manung’uniko ya wananchi kwa vyombo vya mahakama vitakwisha ikiwa mwananchi atatendewa haki mahakamani ipasavyo bila kucheleweshwa pamoja na kupatiwa nakala ya kesi inayomhusu mhusika ili kama ni kukata rufaa kwa mjibu wa   sheria afanye kama inavyotakiwa.
Maadhimisho haya pia yamehudhuriwa na Hakimu mkazi Mfawidhi Wilaya ya Mpanda  Chiganga Tengwa ambaye pia ndiye anayekaimu mahakama ya hakimu Mkazi ya Mkoa wa Katavi,Wakili Adolf Mishanga  mwakilishi wa Shirika la Wwakimbizi la umoja wa mataifa la UNHCR Mishamo,watumishi mbalimbali wa mahakama,wadau mbalimbali wa heria na wananchi.
Hata hivyo licha ya kuwa baadhi ya wananchi walio wengi wameonesha kutotambua maana ya siku ya sheria duniani,baadhi ya waliohudhuria sherehe hizi wameeleza kujifunza mengi ambayo yatakuwa msaada mkubwa katika maisha yao ya kila siku ikiwemo kuzingatia msemo kuwa ‘’Kutofahamu sheria siyo kinga ya kupatiwa adhabu’’
Wakati hayo yakiwa yamejiri Mkoani Katavi,Jijini Dar es Salaa,mgeni rasmi wa maadhimisho hayo Rais Dk.John Pombe Magufuli ameviagiza  vyombo vyote vinahusika katika kutoa haki kuhakikisha vinatoa haki kwa wakati na kwa wale wote wanaoharibu sifa za vyombo hivyo wachuliwe hatua ikiwa ni kiiashirio cha kuanza mwaka wa mahakama hapa nchini.
Aidha Rais ameagiza kuharakishwa kuundwa kwa mahakama ya kushughulikia mafisadi na watu wanaojihusisha na rushwa kwani hatua hiyo ni muhimu kwa maendeleo ya taifa.
Kwa upande wake Jaji  Mkuu wa Tanzania Mhe.Mohamed Chande Othman amesema kuwa wapo katika mchakato ili kuhakikisha mahakama hiyo inafanya kazi kwa mwaka huu wa 2016.
Kauli mbiu katika maadhimisho ya mwaka huu ni  ‘’UTOAJI WA HAKI INAYOMLENGA MTEJA,WAJIBU WA MAHAKAMA NA WADAU.
Nchini Tanzania Maadhimisho ya siku ya sheria yalianzishwa mwaka 1996 ambapo kitaifa mwaka huu yameadhimishwa Jijini Dar es Salaam na Mgeni Rasmi akiwa ni Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli kwa uongozaji mkuu wa Jaji  Mkuu wa Tanzania Mhe.Mohamed Chande Othman.

CHENJI YA SHILINGI 500/=MKAZI SUMBAWANGA AHUKUMIWA MIAKA 10 KWA KUUA BILA KUKUSUDIA.

Posted By:Issack Gerald | At:Saturday, February 06, 2016

Na.Issack Gerald-Sumbawanga
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Sumbawanga mkoani Rukwa imemhukumu kifungo cha miaka 10, mkazi wa kijiji cha Kazila Lizberth Fredinad (21) baada ya kupatikana na hatia ya kumuua Charles Abel bila kukusudia.

Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa Fredinad alimuua Charles Abel kwa kumchoma na kuni tumboni akigoma kumlipa marehermu chenji yake ya shilingi 500 aliyokuwa akidaiwa.
Akisoma hukumu hiyo jana, Jaji Mfawidhi Kakusulo Sambo alisema kuwa anatoa adhabu hiyo kali kwa mshtakiwa huyo ili iwe fundisho kwake na wengine wenye tabia ya kujichukulia sheria mkononi.
Awali Mwendesha Mashtaka, wakili wa serikali Happiness Mayunga alidai mahakamani hapo kuwa mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo Februari 6, mwaka jana na kusababisha kifo.
Ilidaiwa kuwa siku hiyo ya tukio, mshtakiwa huyo aliingia katika kilabu cha pombe za kienyeji ambapo pia palikuwa panachomwa nyama ya nguruwe na kukuta wateja wengine wawili wakinywa pombe hiyo.
Ilielezwa kuwa ndipo marehemu alipoanza kumdai marehemu ampe chenji yake ya shilingi 500 na kusababisha ugomvi kuibuka baina yao na kuanza kupigana.
Kwa mujibu wa Wakili Mayunga ugomvi huo uliodumu kwa muda mrefu kila wakisuluhishwa waliendelea kupigana ndipo mstakiwa alipomchoma tumbo Charles kwa kuni na kumjeruhi vibaya ambapo alikimbizwa katika zahanati kijijini Kaengesa, Manispaa ya Sumbawanga kwa matibabu.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA