JAMII KATAVI YATAKIWA KUTAMBUA HAKI YA ELIMU KWA WATOTO WENYE ULEMAVU
Na.Issack
Gerald-Mpanda
JAMII
wilayani Mpanda Mkoani Katavi imetakiwa
kutambua haki ya elimu kwa watoto wenye ulemavu kwa kuwaandikisha katika shule
zinazotoa elimu maalumu kwa watoto walemavu.
Akizungumza
na P5 TANZANIA MEDIA Afisa elimu kitengo cha vifaa na takwimu wa
halmashauri ya wilaya ya mpanda Bw. Amos Mwasa amesema elimu ni haki ya kila
mtu, hivyo wazazi wenye watoto wenye ulemavu watambue haki ya watoto wao ya
kupata elimu stahiki.
Aidha
Bw. Mwasa amesema baadhi wa wazazi wamekuwa wakiwaficha watoto wao, pasipo
kuwapeleka shule na kuwanyima haki ya kupata elimu.
Amesema
mwitikio wa kuandikisha watoto wenye ulemavu katika shule ya Kakora bado ni
mdogo kwani mpaka sasa wameandikishwa wanafunzi wanane tu.
Comments