HAKIMU MAHAKAMAYA WILAYA YA MPANDA ATOA NENO KWA WANAKATAVI KUHUSU SIKU YA SHERIA FEBRUARI 4,2016.
Na.Issack
Gerald-Mpanda
WAKAZI
wa Mkoa wa Katavi wameaswa kuyatumia vizuri maadhimisho ya siku ya sheria
nchini, kupata elimu inayotolewa na wadau wa sheria ili kuelewa haki na wajibu
wa raia.
Akizungumza
na P5 TANZANIA MEDIA Sambamba na Mpanda
radio leo, hakimu mfawidhi wa mahakama
ya wilaya ya Mpanda Bw. Chiganga Tengwa amesema kila mwananchi anatakiwa
kuzielewa sheria za nchi ili kuepuka malalamiko pindi raia atakapochukuliwa
hatua za sheria.
Akizungumzia
tatizo la kesi kucheleweshwa, Bw.Tengwa amesema kwa mahakama ya wilaya mpanda tatizo hilo halipo na kwamba kesi zote
husikilizwa kwa wakati unaotakiwa.
Uzinduzi
wa siku ya sheria mkoani Katavi umefanyika jana katika uwanja wa kashaulili na
Kauli mbiu ya mwaka huu ni “Utoaji wa
haki unaomlenga mteja,wajibu wa mahakama na wadau”
Kilele
cha maadhimisho hayo yatafikia tarehe 4 mwezi huu.
Comments