WANAWAKE MPANDA WATAKIWA KUJIFUNGULIA HOSPITALINI KUPAMBANA NA VIFO
Na.Vumilia
Abel-MPANDA
Wanawake Wilayani Mpanda Mkoani
Katavi wametakiwa kuona umuhimu wa kujifungulia katika vituo vya afya na
kuachana mila potofu za kujifungulia
nyumbani ili kuzuia voifo visivyo vya lazima.
Wito huo umetolewa na mratibu msaidizi
wa huduma za uzazi na mtoto Wilayani Mpanda Bi.Malietha Sikwila wakati
akizungumza na P5 TANZANIA MEDIA
Ofisini.
Aidha amesema wanawake wengi wamekuwa
wakichelewa kufika hospital mapema kuacha tabia ya kutegemea wakunga ambao
wakati mwingine hawana elimu ya kutosha kumsaidia mama anayejifungua.
Pia amesema mjamzito anapoona dalili
za kijufungua anatakiwa kuwahi mapema kwenye kituo cha afya kwa msaada zaidi.
Comments