DAMU SALAMA YAKUSANYWA MPANDA
Na.Lutakilwa Lutobeka-MPANDA
Wizara ya afya kupitia kitengo cha
damu salama Wilayani Mpanda Mkoani Katavi kimewapongeza wananchi walojitokeza
katika zoezi la uchangiaji wa damu huku kikiwaomba ambao hawajachangia wafanye
hivyo ili kuokoa uhai wa wagonjwa.
Damu salama iliyokusanywa |
Hayo yamesemwa na mhamasishaji wa
zoezi hilo Wilayani Mpanda Bi. Redgunnda Mayorwa wakati akizungumza na P5
TANZANIA MEDIA katika viwanja vya Shule ya Msingi Kashaulili akisema kuwa wananchi
waliochangia damu jana wamepunguza tatizo la upungufu wa damu hospitalini.
Aidha Bi.Mayorwa,amesema,wanawake
wameonekana kutokuwa na mwamko wa sula hilo wakati wao ndio wahanga wakubwa wa
matatizo ya upungufu wa damu kwani hakuna hata mwanamke mmoja aliyejitokeza.
Naye mwenyekiti wa bodaboda Wilayani
hapa Bw.Stephano Mwakapafu amewaomba
wananchi kuendelea kujitokeza katka zoezi la uchangiaji wa damu ili kuokoa
maisha ya wagonjwa hospitalini.
Jumla ya UNITS 25 za damu zimekusanywa jana
Jumla ya UNITS 25 za damu zimekusanywa jana
Comments