WAKUU WA MIKOA,WILAYA NA WAKURUGENZI HALMASHAURI NCHINI WATAKIWA KUDHIBITI MIGOGORO YA ARDHI
Na. OFISI YA
WAZIRI MKUU,
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewaagiza Wakuu wa Mikoa, Wakuu
wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kuhakikisha kuwa wanaongeza
udhibiti na usimamizi wa migogoro ya ardhi kwenye maeneo yao husika.
Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majliwa akisalimia na waakazi Jimboni Kwake Ruangwa |
Ametoa
agizo hilo leo mchana (Jumatano, Desemba 23, 2015) wakati akizungumza na viongozi
wa mkoa wa Lindi kwenye Ikulu ndogo mara baada ya kuwasili akitokea jimboni
kwake Ruangwa.
“Ardhi
ni mali ya Serikali lakini maeneo yanayotwaliwa kwa sababu mbalimbali za
maendeleo yasiwe chanzo cha migogoro na wananchi tunaowaongoza,” alisema.
Akitoa
mfano, Waziri Mkuu alisema anatambua kuna mgogoro wa eneo la mgodi katika
wilaya ya Ruangwa baina ya wananchi na wawekezaji wa kampuni ya Uranex. Na hii
ni kwa sababu wao ndiyo waliamua kufanya tathmini (evaluation) ya eneo hilo.
Yale ni makosa kwa sababu aliyepaswa kufanya tathmini ni Halmashauri na siyo
mwekezaji,” alisema.
Alisema
wawekezaji wanaruhusiwa kisheria kufanya tathmini lakini sheria waliyoitumia ni
sheria namba 8 peke yake. “Kama Halmashauri ingefanya kazi hiyo ni lazima
wangetumia sheria ya ardhi ya vijiji pamoja na sheria ya madini na wananchi
wangepata thamani halisi ya ardhi yao,” alisema.
“Ninaagiza
Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa ikahakiki lile eneo na kubaini kama ni la
kilimo au la madini na kama ni la kilimo, wananchi wamelima mazao gani na kwa
muda gani kisha wafanye tathmini upya. Yuko valuer wa Halmashauri mwenye
dhamana hiyo na siyo wao,” alisema.
“Nasisitiza
tena ni vema Wakurugenzi wote, Wakuu wa Wilaya chini ya uongozi wa Wakuu wa
Mikoa mjiridhishe kuwa hakuna migogoro kwenye maeneo yenu. Kama ipo, imalizeni
kwa kukaa mezani na kuzungumza na pande husika, inawezekana kabisa,”
alisisitiza.
Comments