MKURUGENZI MKUU RAHCO ASIMAMISHWA KAZI
Na.OFISI YA MAWASILIANO YA IKULU.
Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk.John Magufuli
amemsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli
Tanzania (RAHCO), Benhadard Tito.
Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli |
Rais Magufuli amesema,amemsimamisha Bw. Tito kupisha
uchunguzi wa kina kutokana na ukiukwaji mkubwa wa taratibu za manunuzi, yaliobainika
katika mchakato wa utoaji wa zabuni ya ujenzi wa Reli ya Kati.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, Dk
Magufuli,amefikia uamuzi huo baada ya kuitisha kikao cha wataalamu kutoka
wizara na taasisi mbalimbali za serikali, ambazo zinahusika katika utekelezaji
wa Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kati kwa kiwango cha kisasa.
Aidha Rais Magufuli ameivunja Bodi ya Rahco baada ya
kujiridhisha kuwa haikutekeleza ipasavyo wajibu wake katika kusimamia mchakato
wa zabuni hiyo na badala yake imeonekana kutetea kilichofanyika.
Comments