BREAKING NEWS : KAIMU MKURUGENZI WA TAASISI YA SARATANI YA OCEAN ROAD ASIMAMISHWA KAZI


Na.Ofisi ya Waziri-DAR ES SALAAM.
Kaimu mkurugenzi wa taasisi ya saratani ya Ocean Road Dk.Diwani Msemo amesimamishwa kazi.
                                                      
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu amesema,Dk.Msemo amesimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi pamoja na mambo mengine ikiwa ni pamoja na kubaini kama kuna mgongano wa kimaslahi ambao umeathiri utendaji chini ya Kaimu Mkurugenzi.
Wakati huo huo Mh.Ummy,ameiagiza bodi ya taasisi ya saratani ya Ocean Road kuteua mkurugenzi atakayekaimu nafasi ya Mkurugenzi mtendaji.
Katika hatua nyingine,watendaji wote wa serikali katika sekta ya afya wakiwemo wafamasia,wauguzi na waganga wafawidhi wa vituo vya kutolea huduma,wameagizwa kukiri kwa maandishi ikiwa wanamiliki zahanati,vituo vy afya,kliniki na maduka ya dawa ndani ya siku 21 kuanzia leo Desemba 23.
Amesema kuwa agizo hili,halimwondolei wajibu kiongozi yeyote wa serikali ambaye anapaswa kujaza tamko la viongozi wa Umma kuhusu rasilimali na madeni kwa mjibu wa kifungu namba 9 na 11 cha sheria ya maadili ya viongozi wa Umma namba 13 ya mwaka 1995 na namba 5 ya mwaka 2001

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA