WAOMBA KIKAO CHA AMANI KATAVI
Na.Issack Gerald-KATAVI
Mkuu wa Mkoani Katavi ameombwa kuitisha kikao maalumu
kinachojumuisha tume ya taifa ya uchaguzi,wanasiasa na wazee maarufu Mkoani
Katavi ili kujadili namna ya kukabiliana
na viashiria mbalimbali vya uvunjifu wa amani vinavyojitkeza kwa sasa kuelekea
uchaguzi Oktoba 25 mwaka huu.
Ombi hilo limetolewa leo katika kikao
maalumu cha tatu kinachojumuisha wazee maarufu ,wanasiasa na wafanyabiashara
kikao ambacho kimefanyika Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoani Katavi kujadili
mustakbali wa amani Mkoani Katavi kipindi cha kampeni.
Kwa upande wake kaimu kamanda wa
Polisi Mkoani Katavi Rashid Mohamed ametoa wito kwa wakazi MKoani Katavi kutounga
mkono kauli zinazoweza kuligawa taifa.
Wakati huo huo Oktoba 16
imependekezwa kufanyika kikao cha Mkuu wa Mkoa huku kingine cha Kamanda Polisi
Mkoa kikipangwa kufanyika Oktoba 19 mwaka huu
Comments