WAKAZI WILAYA MPYA YA TANGANYIKA WAOMBA HUDUMA ZA JAMII
Wakazi Wilaya mpya ya Tanganyika wakizungumza na P5 TANZANIA Wilayani hapo |
NA.Issack Gerald-TANGANYIKA
Wakazi katika Wilaya Mpya ya
Tanganyika Mkoani Katavi wameiomba serikali ya Mkoa wa Katavi kuongeza huduma
mbalimbali za kijamii zikiwemo afya na Ofisi za Watumishi wa Umma katika kata ili kuondokana na adha ya kupata
huduma umbali mrefu.
Hayo yameelezwa na baadhi ya wakazi
wa Wilaya hiyo wakati wakizungumza na P5 TANZANIA kuhusu chanamoto mbalimbali
wanazokabiliana nazo.
Aidha wamesema mamlaka zinazohusika
Mkoani Katavi zifanye mpango wa mgawanyo wa utawala kata hadi kata ili wajue
eneo wanakotakiwa kupata huduma za jamii.
Baadhi ya maeneo yanayounda Wilaya
Mpya ya Tanganyikia ni Pamoja na Tarafa ya Karema na kata zake.
Tangazo la kupatikana Wilaya ya Tanganyika lilitolewa mwezi Agosti mwaka huu na serikali
ya Jamhuri ya Muungano wa wakati wa kuvunja balaza la mawaziri.
Comments