SIKU YA MWALIMU YAZUNGUMZWA NA CWT KATAVI
NA.Issack Gerald-MPANDA
Chama cha walimu CWT Mkoa wa Katavi
kimesema kimefanikiwa katika masuala mbalimbali yakiwemo udhibiti wa wizi wa
mishahara ya walimu,ujenzi wa benki ya mwamili tangu kuanzishwa kwake.
Siku ya mwalimu duniani ni inaadhimishwa
kiduniani kila mwaka ifikapo Oktoba 05.
Siku hii inalenga zaidi kuangalia
masuala yanayowahusu walimu katika maeneo yao ya kazi ikiwemo utatuzi wa
changamoto zinazowakabili walimu bila
kusahamu kuboresha mafanikio wanayoyapata walimu, haya yote yakifanyika kwa
ajili ya kuinua kiwango cha mtoto ili tupate taifa la leo na kesho lililo imara
na lililoelimika huku suala la ushindani kielimu kati ya nchi hususani nchi
wanachama wa jumuiya ya Afrika ya Mashariki likishika kasi kuumiza vichwa vya
watanzania kuingia katika ushindani wa ajira.
P5 TANZANIA
imezungumza na Mwenyekiti wa Chama cha Walimu CWT Mkoani Katavi John Mshota na
kutaja changamoto zinzowakabili kwa sasa ni pamoja na malimbikizo ya posho na
mishahara ya walimu.
Pamoja na kuzungumzia chanamoto
zinazowakabili Mshota ametaja baadhi ya mafanikio tangu kuanzishwa kwa CWT
Mkoani Katavi ni pamoja na kushiriki ujenzi wa benki ya mwalimu hapa nchini na
kudhibiti wizi wa mishahara ya walimu kwa njia ya mtandao wa benki.
Comments