USHIRIKIANO KATI YA RAIA NA POLISI WAPUNGUZA UHARIFU WILAYA YA MLELE
Na.Issack Gerald- Mlele
Mafanikio ya kupungua kwa uharifu
katika kata zilizopo Wilayani Mlele Mkoani Katavi kumetokana na ushirikiano kati
ya Jeshi la Polisi na jamii inayoishi
katika kata hizo.
Hayo yamebainishwa na mmoja wa waelimishaji
wa elimu ya Polisi jamii katika tarafa ya Mamba kata ya Majimoto Bw.Koplo John
Simba wakati akizungumza na Mpanda Radio kuhusu namna jamii inavyoshirikiana na
jeshi la polisi kupambana na uharifu.
Tarafa ya Mamba ni miongoni mwa
tarafa ambazo zimekuwa zikikumbwa na uharifu wa aina mbalimbali ukiwemo mauaji
ya wanawake.
Comments