TUME YA UCHAGUZI MANISPAA YA MPANDA YAONYA WATAKAOBAINIKA KUANDIKA MAJINA YA WATU NA KITAMBULISHO CHA MPIGA KURA KINYUME CHA SHERIA
Na.Issack Gerald-MPANDA
Tume ya taifa ya uchaguzi Manispaa ya
Mpanda Mkoani Katavi imewataka watu wanaojipitisha katika mitaa mbalimbali ya
Manispaa hiyo kuorodhesha majina na namba za kitambulisho cha Mpiga kura kuacha
tabia hiyo kabla ya hatua za kisheria kuchukuliwa dhidi yao.
Kauli hiyo imetolewa leo na Afisa
uchaguzi Manispaa ya Mpanda Bw.Clavery Reginald wakati akizungumza na Mpanda
Radio kuhusu kukithiri kwa matukio ya kukamatwa kwa baadhi ya watu wakisemekana
kufanya kazi hiyo.
Uchaguzi wa Tanzania unatarajia
kufanyika Oktoba 25 mwaka huu ukishirikisha vyama mbalimbali vya siasa Tanzania
vikiwemo nane katika ngazi ya Urais.
Comments