BAADHI YA VIFAA VYA KUPIGIA KURA VYAWASILI MANISPAA YA MPANDA
Na.Issack Gerald-MPANDA.
Manisapaa
yaMpanda Mkoani katavi imepokea baadhi ya vifaa ambavyo vitatumika katika
upigaji kura Oktoba 25 mwaka huu.
Hayo
yameelezwa na Afisa Uchaguzi Manispaa ya Mpanda Bw. Reginald Clavery wakati
akizungumza na Mpanda Radio Ofisini kwake.
Amevitaja
miongozni mwa vifaa ambavyo vimewasilishwa kuwa ni pamoja na karatasi za kujaza
matokeo ya kura,kalamu,taa na vituturi ama meza za kuandikia
Aidha
amesema kuwa wamepokea karatasi za maandishi nundu kwa ajili ya watu wenye
ulemavu wa kutoona ili kuwawezesha kupiga kura wenyewe kuliko kutumia mtu
mwingine kuwakilisha kura yake.
Comments