WAZIRI MKUU PINDA AKATAA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA KATAVI,AWAACHIA WENGINE KUCHUKUA JIMBO HILO
Waziri Mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda |
NA.Issack Gerald-Mlele Katavi
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amekataa ombi la wananchi wa jimbo
lake la uchaguzi la kumtaka agombee tena ubunge katika jimbo hilo ili
kuendeleza mipango mbalimbali ya maendeleo aliyoianzisha.
Akizungumza baada ya Ibada ya Jumapili katika kigango cha
Kanisa Katoliki cha Kibaoni wilayani Mlele,Waziri Mkuu Pinda amesema
anamshukuru Mungu kwa nafasi aliyopewa ya kulitumikia Taifa akiwa Waziri Mkuu
kwa miaka minane na anaamini wakati umefika wa yeye
kuwaachia wengine nafasi ya ubunge wa jimbo la Katavi.
Waziri Mkuu Pinda Amesema,ataendelea kuwa karibu na wananchi
wa Katavi wakati wote na kwa vile atakuwa na muda wa kutosha atashiriki
kikamilifu katika mikakati mbalimbali ya kuwaletea maendeleo wananchi ili
waweze kujikwamua kutoka kwenye umaskini.
Waziri Mkuu yuko kijijini kwake Kibaoni, wilayani Mlele kwa
ajili ya mapumziko mafupi.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda alikuwa miongoni mwa makada 42 wa CCM
waliokuwa wametangaza kugombea urais wa Tanzania Kupitia Chama cha Mapinduzi ikiwa
angeteuliwa na chama chake ambapo hata hivyo John Pombe Magufuli mbunge wa
Chato Mkoani Geita alipitishwa na chama hicho kuingia kinyang’anyiro cha urais
Oktoba 25 mwaka 2015.
Comments