KATAVI KUMALIZA MIGOGORO YA ARDHI KATIKA MIPAKA YAKE YA UTAWALA
Na.Issack Gerald-Katvi
SERIKALI Mkoani Katavi imedhamilia Kumaliza Migogoro ya Aridhi
kwa Kuweka utaratibu Utakaoishirikisha Jamii ambayo ndiyo huathiriwa Zaidi na
Migogoro hiyo pale inapokuwa imetokea.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dr Ibrahim
Msengi wakati akitambulisha utaratibu Mpya utakaotumika Kukabiliana na Uhalibifu wa Mazingira
uliokithiri Mkoani Hapa.
Dr Msengi amesema kuwa,Utaratibu kama utasimamiwa Vizuri
utasaidia Kupunguza Migongano iliyopo Katika Jamii na Kuufanya Mkoa wa Katavi
Kuwa Mkoa wa Kuigwa na Mikoa yenye Migooro ya Aridhi Nchini.
Mkoa wa Katavi ni Miongoni mwa Mikoa hapa Nchini
inayokabiliwa na Uhalibifu Mkubwa wa Mazingira Kutokana na Kuwa na Idadi kubwa Wakazi Jamii ya Wafugaji wanaohama.
Comments