MPANDA GIZA NENE SUAL LA UMEME,TANESCO YASEMA UMEME KUTENGAMAA MIEZI MITATU IJAYO
Mafundi wakiwa katika matengenezo ya mitambo ya Tanesco Mpanda |
NA.Issack Gerald-Mpanda Katavi
SHUGHULI Za Uchumi Mkoani Katavi zimesimama kwa siku sita
sasa Kutokana na Kukosekana kwa nishati ya Umeme.
Kukosekana kwa Nishati
ya Umeme Mkoani hapa Kwa Muda Usiojulikana kumesbabisha Kupanda kwa Gharama za
Maisha kutokana na shughuli za Uzalishaji zinazotegemea nishati hiyo kusimama
ikiwemo Usafirishaji na viwanda vya ubanguaji na kusindika mazao.
Akizungumza Katika Mahojiano Maalum na P5
TANZANIA Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania Kituo cha Mpanda Bwana,Chacha
Nsiku amesema hivi sasa Juhudi
zinazofanywa na Shirika hilo ni
Kuhakikisha Maeneo ya Huduma Muhimu za Jamii Kama hospitali zinapata umeme.
Aidha bwana Nsiku
ameongeza Kuwa sababu ya Kukosekana kwa Umeme imetokana na Uchakavu wa Mashine
zinazotumika kwa sasa ambapo tatizo hilo litadumu kwa Kipindi cha Miezi Mitatu
kabla ya Kupatiwa Ufumbuzi.
Comments