WALIMU WAPYA MPANDA WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA KUZINGATIA WELEDI,KUTOJIHUSISHA NA ANASA KAZINI
Na.Amosi
Venance-Mpanda Katavi
WALIMU wa
sekondari wilayani Mpanda mkoani Katavi wametakiwa kuwa na maadili na kufuata weledi
katika utendaji kazi ili kuboresha kiwango cha elimu mkoani Katavi.
Afisa elimu
sekondari Bi. Lutungulu Enelia wilaya ya Mpanda ametoa
wito huo jana katika semina iliyofanyika katika shule ya sekondari Mwangaza
iliyopo mjini Mpanda.
Bi. Lutungulu amesema kuwa walimu ni kioo cha jamii hivyo wanapaswa
wawe na maadili katika utendaji kazi.
Aidha amewaasa kujiepusha
na vitendo visivyostahili ikiwa ni pamoja na baadhi ya walimu wasio na maadili
kujihusisha na maswala ya rushwa, ngono, na ukosefu wa nidhamu kazini.
Semina hiyo
imehudhuriwa na walimu wa shule za sekondari wapya 52 walioripoti katika
halmashauri ya mji wa Mpanda.
Comments