KATAVI YATANGAZA VITA DHIDI YA MAUAJI YA WATU WENYE UALBINO TENA


Remi  Luchumi(30) mkazi wa Mwamachoma   Tarafa ya Mamba Wilaya ya Mlele akiwa hospitali ya Wilaya ya Mpanda baada ya kukatwa mkono mwezi juni mwaka huu




Na.Issack Gerald-Katavi

HALMASHAURI ya wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imeweka mikakati ya kukomesha mauaji dhdi ya watu wenye albino.
Taarifa iliyotolewa na Mganga  Mkuu wa hospitali ya wilaya ya Mpanda Dk. Joseph Msemwa ilionesha kati ya mikakati hiyo ni pamoja na kuhakiki waganga wa jadi wanaofanya kazi bila vibali na wanaopiga ramli kufutiwa leseni zao.
Dk. Msemwa alisema kuwa, mikakati mingine ni kuwatambua watu wenye ualbino na kutoa elimu kwa umma ya  kukomesha mauaji ya kikatili, ili iwe ajenda ya kudumu.
Mwezi Juni mwaka 2015 watu wanane walifikishwa  na kupandishwa kizimbani  katika Mahakama  ya Wilaya ya Mpanda  Mkoa wa Katavi  kujibu shitaka  la kumjeruhi kwa mapanga  na kisha kumkata  mkono  na kutomomea nao wa   mwanamke  mmoja aliyetwa Remi  Luchumi (30) mkazi wa Mwamachoma   Tarafa ya Mamba Wilaya ya Mlele na kisha kutokomea nao.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA